Ligi yetu ingekuwa ni ya haki kuna muda Simba na Yanga zisingeongoza ligi

Ligi yetu ingekuwa ni ya haki kuna muda Simba na Yanga zisingeongoza ligi

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Nikifuatilia ligi kuu ya Uingereza naona matimu makubwa kama Man utd, Chelsea, Man City , Arsenal nk yanavyoteseka bila kujali ukubwa wao kwa wingi wa Mashabiki na Fedha .

NImegundua wenzetu wa Ulaya HAKUNA MAELEKEZO KWA MAREFA KUWA MECHI HII LAZIMA FULANI ASHINDE

WENZETU WAMENYOOKA SANA.

Sisi huku inaonekana kama ni dhambi timu zingine kuzifunga Simba na Yanga , inaonekana dhambi timu nyingine kuchukuwa ubingwa isipokuwa Simba na Yanga tu.

1. TFF , Wadau wa soka na wanasiasa hebu acheni timu zipambane zenyewe kwa haki.


2. Viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga acheni kuzirubuni timu ndogo. Pia acheni kuwarubuni waamuzi.

3. Wachezaji wazawa kwa timu zote acheni kuzihujumu timu zenu sababu ya mahaba ya usimba na uyanga (Tunawaona sana mnapocheza na hizi timu kubwa).

Unakuta beki anajidai kuukimbiza mpira unaoelekea golini kwake halafu hata haongezi speed kuuwahi mpira hadi unavuka mstari wa goli na yeye kujilaza chali kuwa amepambana sana, mwingine tunaona anacheza rafu ya makusudi tu ili ipatikane penalty au atolewe kwa red card.

1. TFF IKIAMUA LIGI YETU INYOOKE KWA MISINGI YA HAKI INAWEZEKANA KABISA.

2. TAKUKURU / SERIKALI IKIAMUA KUKOMESHA RUSHWA MICHEZONI INAWEZEKANA MPIRA WETU TZ UKAWA WA MAANA SANA
 
Acha utaahira wako, Yanga kafungwa na Azam,kafungwa na TABORA united,kama kusingekuwepo na fairness basi Tabora na Azam walistahili kufungwa na Yanga. SIMBA VS DODOMA,SIMBA VS JKT,SIMBA VS AZAM,SIMBA VS MASHUJAA. rejea hizo mechi za Simba ndio utagundua timu ipi inabebwa na waamuzi.
 
Back
Top Bottom