Ligu Kuu Uingereza: Chelsea na Tottenham zatawala kikosi bora Ligi Kuu Msimu huu

Ligu Kuu Uingereza: Chelsea na Tottenham zatawala kikosi bora Ligi Kuu Msimu huu

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
_95709613_premier-league-xi-6dbd09d5cbf98203a4e4dc29016c3017.jpg

Chelsea na Tottenham zimetawala kikosi cha wachezaji 11 bora wa Ligi ya Premia msimu huu ambacho kimetangazwa na Chama cha Wachezaji wa Soka ya Kulipwa Uingereza.

Klabu zote mbili zina wachezaji wanne katika kikosi hicho.

Mabeki Gary Cahill na David Luiz pamoja na viungo wa kati N'Golo Kante na Eden Hazard ndio wachezaji wa Chelsea waliojumuishwa kwenye kikosi hicho.

Tottenham inawakilishwa na mabeki Kyle Walker na Danny Rose, kiungo wa kati Dele Alli na mshambuliaji Harry Kane.

Mlindalango wa Manchester United David de Gea, Sadio Mane wa Liverpool na mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku pia wamo kwenye kikosi hicho.

_95709615_championship.jpg

Kikosi bora cha msimu huu katika Ligi ya Daraja la Pili pia kimetangazwa ambapo wachezaji wanne wa klabu iliyopandishwa daraja hadi Ligi Kuu ya England, Brighton wakiwa kwenye kikosi hicho.

Wachezaji hao ni golikipa David Stockdale, mabeki Bruno and Lewis Dunk na mchezaji bora wa msimu ligi hiyo, kiungo wa kati Anthony Knockaert.

Newcastle wana wachezaji watatu: beki Jamaal Lascelles, kiungo wa kati Jonjo Shelvey na mshambuliaji Dwight Gayle. Chris Wood wa Leeds, mfungaji mabao bora ambaye ametikisa wavu mara 25 pia ameteuliwa.

Fulham wana wachezaji wawili katika kikosi hicho - beki Ryan Sessegnon na Tom Cairney, ambaye yumo safu ya kati na mchezaji wa Huddersfield Aaron Mooy.

Chanzo: BBC Swahili
 
Alexis Sanchez hayupo, Sikubaliani na hiyo List
 
Hapo kwa Mane wengeendelea kumuweka tu Moses.....
 
Uwepo wa kante ilhali pogba au felaini hawapo inatia shaka kamati ya masaa 72 iliyoteua hicho kikosi.
 
Kama wangeangalia nafasi ya timu basi wote watoke chelsea...
Chelsea wa 4,totti 4 timu mbili za juu zimetoa wachezaji 8, nafasi 3 ndo moja liva,man utd,na everton. Wengi tu wazur wamebaki sema ndo wanahtajk 11,mfano sanchez,zlatan,coutinho nk pia wameperform vzr tu.
 
Jiunge na group la whatsap la betting lenye members zaidi ya watu 130 upate mikeka ya uhakika na ushauri mzuri kuhusu mechi na company za betting. Kujiunga ni bure na ushauri na mikeka yote ni bure. Linki iyo hapo chini.<br /><br /><br /><br />Betting only
 
Back
Top Bottom