Lijishangazi au kademu, nimuoe nani?

Myebusi Mweusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2022
Posts
671
Reaction score
1,543
NANAOMBA USHAURI

Habari yako mwana JF mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 ninafanya kazi ya bodaboda

Nilikuwa na mpenzi wangu niliyeishi nae kwa miaka 4 sasa na tuna ahadi ya kuoana

Lakini mwaka juzi nilipata abiria MAMA mtu mzima ana miaka kama 45 ni mtu anayejiheshimu na anafanya kazi ya kuuza genge (matunda,nyanya, dagaa na vitu vyengine) tulianza mahusiano ya kibiashara kama bodaboda wake kisha akawa mshauri wangu yaani nikipata tatizo la kutaka ushauri huwa namuona yeye na ananishauri vizur mno maisha yamekwenda hadi akawa mpenzi wangu

Tokea tuwe wapenzi amekuwa mtu muhimu sana katika maisha yangu amenishaur mambo mengi hadi sasa najiona nimepiga hatua kubwa ya kimaisha mwanzoni nilikuwa na pikipiki moja lakin sasa hivi ninazo mbili na pia nimefungua biashara ya kuuza chips na pia nimefungua machine za kuuza juice ya miwa ninakwambia ukweli kabisa mawazo yote haya yametoka kwa huyu mwanamke. Mwanzoni hela yote nilikuwa naimaliza kwa mirungi, kubeti na pombe nashukuru kwa ushauri wake mirungi na kubeti nimeacha kabisa pombe nayo naelekea kuacha kabisa haya yote ni mawazo yake na ushauri wake

Changamoto imekuja kuwa anataka tuoane na mimi sijawahi kumwambia kuwa nina mpenzi mwengine kwa sababu mara nyingi huwa nina lala kwake (mpenzi wangu anaishi kwao)

Napata wakati mgumu wa kufanya maamuzi nifanyeje??

Nampenda huyu Mama kutokana naamini nikiendelea kuwa nae maisha yangu yatazidi kuwa mazuri kutokana na mawazo yake

Lakini pia yule mpenzi wangu nae nampenda sana na ananipenda na nyumbani kwao wananijua japo sio rasmi

WOTE NAWAPENDA SIJUI NIFANYE NINI??
 
Kuna thread humu ya tarehe 01/05/2024, dogo anaitwa moja mbili tatu anaomba mbwinu za kuwanasa mishugamami aka mishangazi.

Moja ya mbwinu aliyopewa ni kuendesha boda boda kama Myebusi Mweusi na huko atakutana na mishugamami.

Hongera dogo kwa kukipata, lakini hapo kwa mshangazi huna future kwa sababu huna raha naye na pili bado una tamaa hujui ubaki na yupi.

Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Huyo wa 45 anakaribia au ameshaingia menopause ,hivyo kupata watoto sahau .

Wewe bado kijana ,tafuta kijana mwenzako ,huyo wa 45 miaka yote alikuwa wapi mpaka akose mume wa kumstiri ?
 
Treni inaacha reli.
Huyo mama ana watoto? Kama anao wangapi? Umesema miaka 45, hivi menopause huwa ni miaka ngapi wakuu?
 
Shangazi hajafika menopause kweli? Anashika mimba?
Una mtoto au una mpango wa kuanzisha familia au utarithi watoto wa shangazi ambao mmepishana miaka 10? ?

Oa kijana mwenzako. Shangazi abaki mshauri wa ndanni wa familia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…