Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Katika karne ya 19 wakati huo China ikitawaliwa na mfalme (Kipindi cha Qing Dynasty), Serikali ya China ya wakati huo ilitafuta fedha za kujenga reli kutoka jimbo la Hunan hadi mji wa Guangzhou.
Ili kupata fedha iliamua kuuza treasury bonds kwa watu wa nchi za West, wakiwemo wamarekani, waingereza, wafaransa na wajerumani. Bond hiyo ilibidi iwe ya miaka 40 na riba ya 5% kila mwaka.
Baada ya kuanguka ufalme, serikali ya China iliyofuata (Republic of China) iliendelea kulipa deni mdogomdogo
Hata hivyo baada ya kutokea vita vya wenywe kwa wenyewe na matokeo yake chama cha Kikomunist cha China chini ya Mao Ze Dong kutwaa madaraka ya kiutawala, serikali ikagoma kulipa deni hilo.
Hata hivyo serikali hiyo ya China ilibanwa na uingereza mwaka 1987 chini ya mwanamama Margreth Thatcher kuwa iwapo China haitolipa deni hilo kwa wananchi wa Uingereza walionunua bond hizo basi haitofungua soko la Uingereza kwa China na pia Uingereza ingeweza kusitisha mpango wake wa kuirudisha Hong Kong kwa Uchina. Wachina wakalipa waingereza takriban dola milion 23
Hata hivyo Wachina wakaendelea kugoma kuwalipa wananchi wa Marekani mpaka sasa. Sasa hivi wamarekani wenye kudai wamelivalia njuga suala hili na wanataka serikali yao ihakikishe China inalipa hili deni.
Iwapo China italipa hili deni, basi linakaribiana sana kiukubwa na deni ambalo wachina wenyewe wanaidai Marekani katika masuala hayohayo ya treasury bonds.
Kwa maelezo zaidi sikiliza hii clip: