Lijue soko la HISA

Ma
Majibu tunasubiria tafadhalii...
 
Asante kwa elimu. Naomba utusaidie maana ya maneno unayoyatumi eg dividend, securities, mfano mimi najua security ni usalama, mlinzi wa usalama???
 
Somo zuri sana una nikumbusha mwaka wa pili chuo
 
Deadline lini ya kuacha Kuuza
 
Uzi mzuri sana, kuna kipindi kaa miaka mitano iliyopita nilitaka kununua hisa za CRDB, mtu nilie mfata kumwomba ushauri akanivunja moyo but nilikuwa nimejipanga ila one day ntazinunua tuu
 
Mkuu somo hili zuri sana, lina kila jibu la maswali yanayohisiana na Hisa na kadhalika. Nikuombe ushauri kwa watu kama mimi tuliowahi kununua Hisa za NICOL ambayo hatimaye imefutwa ama kujifuta kwenye soko la Hisa. Matarajio kutokana na uhamasishaji uliofanywa ndani ya nchi na nje kwenye Balozi zetu yalifanya watu wawe na imani hivyo wakajiunga kwa wingi. Kuyeyuka kwa NICOL kutakuwa kumewavunja moyo wadau na kama inawezekana kujua ilikoishia na kupewa ushauri kutaamsha ari ya wahusika kujaribu kwingine kwa kutumia SOMO ulilotoa. Kama ni wewe mkuu au yeyote anayefahamu naombeni ushauri
 
Kampuni gani unaizungumzia hapa???tuangalie possibility ya kuwekeza
 
Mada ya msingi imetuelimisha kuhusu Hisa. Kinachofuata wadau ukisikia tangazo jiulize maswali yote au machache kwa kufuata mifano aliyotoa ili ujiridhishe kuinunua Hisa husika. Angalizo aliyotoa litufungue ili tuweze kuona mwisho kutokea mwanzo vinginevyo utajiingiza kwenye mlango usiohusika.
 
Asante kwa elimu. Naomba utusaidie maana ya maneno unayoyatumi eg dividend, securities, mfano mimi najua security ni usalama, mlinzi wa usalama???
Dividend ni gawio la hisa na security ni usalama ndio ila unaongelea usalama katika uwekezaji wa pesa. Na ili pesa iwe salama tunakuwa tunawekeza kwenye mali zinazotoa gawio ili kulinda thamani ya pesa zetu. Ndo mana mali zinazowekezwa huwa tunaziita security.
 
Fursa ya kidigitali ipo hewani

Angalieni fursa hii pamoja na mjadala unaoambatana nao kwa manufaa yenu na vizazi vyenu vijavyo katika karne hii ya kidigitali.

Mambo yakienda kama yalivyopangwa, utapata fursa ya kushiriki kwenye soko la hisa la kimataifa ukiwa kama mmiliki anayeuza hisa zake ambazo utazipata kwenye mradi huu bila ya kulipia hata senti tano.

Kwa wale wasioogopa kuthubutu
 
Ninaomba mwenye elimu juu ya uwekezaji katika hisa,kwanza nini maana ya hisa?inafanyaje kazi? Faida zake zikoje? Ninaomba unielezee kwa mifano
 
Ukitaka elimu hii vzur kabisaa nenda mlimani city duka la vitabu utakita kitabu Kimeandikwa Hisa,akiba na uwekezaji mwandishi Emilian busara,huyu ni mtanzania aliyefanikiwa saana katika mambo ya Hisa tena anawekeza Tanzania,ana vitabu vingi bei sh 5000 mimi nimejifunza kwake na nawekeza umojafund,na mifuko mingine,
 
Asante mkuu kwa elimu mimi nipo interested na threads za namna hii
 
Naomba ushauri nilinunua hisa 50 mwaka 1995 kwa 25,000/= kwa hisa moja,nikapewa satifiketi ya umiliki huo,Nyumba niliyokuwa naishi iliungua Moto na kila kitu ndani kiliteketea,Sa nikitaka kufuatiria hisa zangu hizo nifanye nini....??hisa hozo ni za TBL.....NAOMBA USHAURI.....
 
Davion Delmonte Jr.
mkuu naomba nisaidie, je ninahitaji niwe na kiasi gani kuanzia kununua hisa, au minimum natakiwa kununua hisa ngapi?

je muda minimum wa kuuza hisa ni siku ngapi baada ya kununua hisa?
ahsante.

Kiasi chochote unaweza kutumia kununua hisa. Ila ingependeza ungekuwa unataka kujua unanunua hisa kwa dhumuni lipi hasa.
1. Unaweza kununua hisa kwa bei ya chini ili uuze bei ikipanda.
2. Unaweza kununua hisa kwa ajili ya kupata gawio.
Ukiwa na hisa nyingi ndo unaweza ku-maximize returns.
Pia, unaweza kufikiria financial products nyingine ambazo zipo more stable and profitable.
 

1995 hizo hisa ulinunulia wapi?
 
ahsante mkuu, je ni financial products zipi ambazo ni more profitable?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…