Likawage Wilaya ya Kilwa (Lindi) inadaiwa kuna changamoto ya mawasiliano, watu wanapanda milimani kupata mtandao

Likawage Wilaya ya Kilwa (Lindi) inadaiwa kuna changamoto ya mawasiliano, watu wanapanda milimani kupata mtandao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Katika maisha yetu ya kila siku, mawasiliano hutusaidia kujenga uhusiano kwa kuturuhusu kushiriki uzoefu wetu, na mahitaji yetu, na hutusaidia kuungana na wengine. Ni kiini cha maisha, huturuhusu kuelezea hisia, kupitisha habari na kubadilishana mawazo. Sote tunahitaji kuwasiliana.

Hata hivyo katika baadhi ya maeneo Tanzania kumekuwa na changamoto za kupata mawasiliano, hatua inayowakosesha Wanachi haki yao ya msingi ya kuwasiliana.

Kata ya Likawage, Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi inachangamoto ya mtandao hasa Vijiji vya Nainokwe na Liwiti.

Hali ambayo inasababisha watu kujitega sehemu na wengine kupanda milimani ili kupata mawasiliano ambayo nayo yanapatikana kwa kukatikatika.

Tunaomba serikali iboreshe mawasiliano ili tuwe tunaongea na simu hata tukiwa ndani ya nyumba.
 
Mitwero tu yenyewe hapo mji mpya km 10 mpk mjini kuna shida ya mtandao.
 
Nakumbuka mwaka 2010 ndio ilikuwa kabisa hakuna usafili wenyewe zilikuwa canter au Yale makubota ya kulimia kumbe mpk Leo hakuna mawasiliano
 
Back
Top Bottom