Mimi pesa ninayo nimetoa maoni tu.
Kuishia kuonesha pesa kwenye mtandao ni ulimbukeni tu wa ujana.
Ulishaona wale matajiri watu wazima wenye busara zao wanaojulikana wanaonesha pesa hadharani mtandaoni ?
Sio vema kwa mtu mwenye busara kuonesha maburungutu hadhalani wakati kuna watu masikini hata uwezo wa kupata uji wa unga wa muhogo unawashinda.
Nazungumzia watu masikini na sio wewe na mimi, watoto wa mitaani, waliotelekezwa na familia, wakimbizi wa vita, wagonjwa.
Nenda Darful ukaone jinsi watu wanavyo jianika jangwani wakisubiri kufa kwa kukosa maji na chakula.
Nimesema Sio Vema Kwa Watu Wenye Busara Kufanya Hivyo, Nadhani Umenielewa.