Likizo yangu na niliyoyaona

Likizo yangu na niliyoyaona

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Nilikuwa likizo ya mwaka kuanzia tarehe 15/10/2012 hadi tarehe 12/11/2012.Ni likizo ya siku ishirini na nane. Wakati wa likizo hii,nilijielekeza katika kutembelea ndugu,jamaa na marafiki huku nikisadifu maendeleo ya nchi hii katika sehemu husika. Ni maendeleo yenyewe hasa na si yale wanayotambia wanasiasa Bungeni,majukwaani na kwenye vyombo vya habari.

Nilifanikiwa kutembelea mikoa ya Mtwara(Mtwara Mjini),Kilimanjaro(Moshi Mjini na Rombo),Ruvuma(Songea Vijijini),Manyara(Simanjiro) na Tanga(Tanga Mjini,Lushoto,Bumbuli,Korogwe,Muheza na Handeni). Nilivyoviona kwa kifupi:

1.Maendeleo ya kiuchumi. Karibu sehemu hizo zote,wananchi bado wako kwenye hali tete ya kiuchumi hasa katika Wilaya za Mkoa wa Tanga. Kiufupi,hali ni mbaya:hata mlo mmoja ni kazi kuupata.

2. Maendeleo ya Kisiasa.Sasa siasa za upinzani zimeshika kasi.Nimekuta kuimarika kwa vyama vya upinzani hasa CUF(Tanga) na CHADEMA(Ruvuma na Mtwara).Ni jambo la kupigiwa mfano. Ieleweke kuwa katika mikoa mingine kama Manyara na Kilimanjaro upinzani ulishaanza kitambo.

Nitaendelea wakuu,nimepata dharura kidogo hapa niishipo...
 
poa mkuu tunaendelea kukusubiri welcome back aisee..
 
Back
Top Bottom