Lil Wayne akumbwa na ugonjwa wa kifafa tena, azimia ndani ya ndege

Lil Wayne akumbwa na ugonjwa wa kifafa tena, azimia ndani ya ndege

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
xlil-wayne.jpg.pagespeed.ic.XjFmHxlI3X.jpg



Star wa muziki nchini Marekani Lil Wayne ameshambuliwa kwa mara nyingine tena na ugonjwa wa kifafa.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, ndege binafsi aliyokuwa amepanda rapper huyo, ililazimika kutua kwa dharura huko Omaha, Nebraska Jumatatu hii. Weezy alikuwa akisafiri kutoka Milwaukee kwenda California pindi tukio hilo lilipotokea.

Wayne alidaiwa kuzimia akiwa kwenye ndege na kupewa huduma ya kwanza. Hata hivyo ripoti zimedai kuwa alikataa kutibiwa. Taarifa zimedai kuwa alipata tena kifafa cha pili baada ya ndege yake kupaa na ililazimika arudishwe Omaha. Alipoteza kabisa fahamu na alipelekwa hospitali kwa ambulance.

Tunechi aliwahi kupata tatizo kama hilo mwaka 2012 baada ya ndege binafsi kutua kwa dharura kwa siku mbili mfululizo.

Pia aliwahi kupata kifafa kikali mwaka 2013.
 
Anakataa kutibiwa kwa nini sasa! Au ndio NDAGU ZAKE
 
Syrup(sizzurp) is not good for your health, weezy hii kitu itakuja kumuua
 
Back
Top Bottom