Mengi Ayoub
Member
- Apr 20, 2022
- 56
- 46
Mwandishi: J.K.kiimbila
MFALME BINTA NA RAIA ZAKE _1
Hadithi hii inaanza Zama za Giza _ jina la kukebehi katika Afrika. Wakati wanadamu walipoabudu miungu wengi lakini wakaendelea kuamini juu ya Hawa miungu palikuwepo Mungu mkuu. Wakati watu walipoamini waganga. Walipopiga ramli. Walipofanya matambiko ya kila namna. Hadithi hii inaanza na nchi ya utamaduni.
Mfalme BINTA alipoanza kutawala utamaduni, nchi yake ilikuwa maskini Sana. Lakini mfalme akatambua faida ya kazi. Hivyo akawahimiza raia wake wafanye kazi kwa bidii. Kila raia akawa mtumwa wa kazi. Kazi ikajenga maisha ya watamaduni. Kwa sababu ya kazi ngumu, nchi ilistawi na kufika kilele Cha mafanikio ambacho hakijapata kufikiwa. Lakini Sasa baada ya miaka kupita , utajiri mwingi ulianza kuleta walakini katika maisha ya mfalme BINTA , mfalme akavutwa mno na utajiri . Moyo wake haukutulia bila kuona Mali nyingi ikimjia kila siku. Akaona Mali aliyonayo haimtoshi . Akawa na kiu ya Mali .Akazidi kutaka Mali zaidi . Kadri alivyopata Mali ndivyo ndivyo alivyozidi kutumbukia kwenye Lindi la anasa , mwishowe akawa mchoyo . Akaanza kunyang'anya raia Mali zao na kujaza tumbo lake tu. Hakutoshoka na hayo akaanza kula rushwa na kuuza haki za raia zake . Bila kutoa rushwa , usingalifanikiwa Jambo lako. Raia wale wenye vitu vya thamani walidhulumiwa , wakapokonywa Mali zao na pengine kuuawa. Mali zao zote zikafanywa Mali ya mfalme . Hatimaye mfalme ikawa haoni karaha kufanya Jambo lo lote lililo baya .
Ingawa raia maisha yaliwaenda mrama , kwaajili ya uonevu wa mfalme, lakini walinung'unika kwa ndani bila kutoa malalamiko yao kinaganaga. Waliogopa kupoteza maisha yao.
Moyo wa mfalme uliendelea kudidimia katika Mali na anasa . Anasa zikamfanya mfalme aache mapokeo mazuri ya Babu zake , akawa na itkadi katika ulozi wa kila namna . Usingizi mfalme hakuupata . Kila siku ikawa yeye kulala usingizi wa mang'amung'amu akiwaza na kuwazua namna angalitajirika kuliko ye yote yule.
Inaendelea sehemu ya 2
=========
SEHEMU YA PILI
MFALME ATAFUTA MALI:
Baada ya siku nyingi za taamuli , wazo la hekima Kama mfale alivyoliona lilimjia. Aliwakusanya waganga wake akawaamuru watafute njia ya kumaliza matatizo yake. Waliagizwa wapige bao na watoe taarifa jinsi Mali nyingi inavyoweza kupatikana .
Kazi hii waganga walipofanya vizuri Sana , kwasababu shetani aliwasaidia . Baada ya siku chache , waganga walitoa taarifa kuwa kila kitu kitakuwa timamu. Walimwambia mfalme kuwa Mali yaweza kupatikana ikiwa mfalme atapata mkia wa Jitu. Kama mkia wa Jitu ungalipatikana Basi mfalme angalipata chochote akitakacho. Mfalme kusikia vile Basi furaha yake haikuwa kifani , alimradi ua la moyo wake lilichanua kwa kufikiria utajiri ambao angalipata.
Siku ya pili mfalme aliamrisha mbiu ya mgambo ipigwe. Naam , mbiu ya mgambo ikalia kila sehemu , mashujaa wote wenye nguvu walitakiwa. Mara mashujaa walikusanyika kwenye boma la mfalme . Wote waliokelewa kwa taadhima waliostahili. Mfalme aliamka katika kitu chake Cha enzi na kumuamuru waziri mkuu atoe hotuba, waziri mkuu akaanza 'Mfalme mtukufu wa utamaduni , mabwana waheshimiwa na mabibi, . Katika Baraza Hili wamealikwa mashujaa wote , mfalme anataka hao mashujaa wasahau nafsi zao, wajitoe sadaka na kumtumikia . Anatakiwa, kwa kweli mtu mmoja , Tambo la mtu . Tena mtu hodari . Mtu ambae yuko tayari kujitoa sadaka na kukabili kifo . Je yuko shujaa yeyote aliye tayri kumsaidia mfalme ?
Mashujaa kwa sauti moja walisma "SOTE TUKO TAYARI" "Ahsante raia wa mfalme" aliendelea yule waziri , "Ahsante Sana kuonesha moyo wa uzalendo kwa kumkinga mfalme mtukufu binta . Basi jitayarisheni kushika ombi la mtukufu . Kazi inayotakiwa ni kusafiri katika nchi ya ujinini , kumwagika Jitu mmoja , kumkata mkia na kuuleta mbele ya mfalme . Je mko tayri kumsaidia mfalme? "
Watu kusikia vile walivuta pumzi za woga . Macho yao yakawatoka Pima kwa woga Kama kwamba yatadondoka. Wakasimama kimya na dunia yote ikawainamia kwa kusikia hatari isiyoshindika. Kwa muda wa dakika tank hakuna aliyeweza kusema au kukohoa . Wote walijaa khofu ya kifo , na midomo yao ikabaki wazi kwa woga . Hata wale mashujaa wajulikanao kwa Vita , walitafuta ardhi ya kuwameza. Kukubali kumwinda Jitu ni sawasawa na kukubali kutoa kichwa chako mdomoni mwa Simba . Nani angekubali kutia kichwa chake mdomoni mwa Simba ? Nani angekubali kuyakaribia majitu? Majitu yaliotoka ndimi za Moto. Majitu yenye mbio za Kasi Mara mbili kuliko mwanadamu. Majitu yaliyopewa nguvu za majini. Hakuna shujaa hata mmoja aliyejitolea.
Hapa ndipo aliposimama madua , shujaa wa Kwanza wa nchi . Madua akasema bila hofu kuwa Jambo la namna hiyo haliwezekani . Akasema kuwa hakuna mtu hata mmoja angalikubali kujifanya mganga kwa kifo ambacho ni bayana . Maflme kusikia maneno hayo , akakasirika Sana akaamuru kichwa Cha madua kikatwe. Kufumba na kufumbua , madua alilala chini mauti. Wakati hayo yote yakitokea hakuna aliyejimudu Wala kusema neno .
Mfalme alipoona ya kuwa watu wote wapo kimya na kimya kingi kina mshindo , akang'amua Mara moja kuwa jshawishi wa waziri mkuu haujafua dafu . Basi akatoa amri kuwa raia wasambae na wabaki mashujaa maarufu kumi wa mwanza wajulikanao katika nchi ya utamaduni. . Baada ya watu kusambaa mfalme akatoa amri kuwa MPILI , shujaa wa pili wa utamaduni atake asitake lazima asafiri mpaka ujinini kuukata mkia wa Jitu . Habari hii ilipotolewa , kila mmoja alimsikitikia Sana mpili . Kila mmoja alimwona Kama marehemu .
Msomaji anaweza kukisia Hali ya mpili baada ya amri kutolewa . Ikiwa mashujaa ambao hawakuhusika na kwenda kuutafuta mkia wa Jitu waliogopa , sembuse mpili mwenyewe ?
Itaendelea sehemu ya tatu