Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Mtangazi wa Wasafi FM kituo kinacho milikiwa na Joseph Kusaga amefunguka wazi yeye awezi kamwe kumtafuta msanii yeyote yule amfanyie interview hasa Nandy.
Mtangazi Lily Ommy amesema wazi kabisa kuwa amekuwa akimuona Nandy ana landa landa tuu mtaani kamwe awezi kumtafuta amfanyie interview labda Nandy au meneja wake wamtafute yeye.
Mtangazaji Lily Ommy aliyasema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na moja ya TV za mitandaoni ambao walitaka kujua maoni yake kuhusu muziki wa Nandy na kwanini hajawahi kufanyiwa interview Wasafi FM.
Mtangazaji huyo mwenye swaga za kimarekani alionekana kukerwa sana na swali hilo kuhusu Nandy na Mziki wake.
Ikumbukwe kwamba Msanii Nandy alikuwa mkubwa kabla hata ya Kusaga kupanga kuanzisha kituo cha Wasafi FM. Pia, kwa sasa Nandy anafanya show yake ya Nandy Festival akizunguka mikoa tofauti Tanzania.
Ni hayo tuu