Linah: kwa heri Tanzania house of talents(THT)

Linah: kwa heri Tanzania house of talents(THT)

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mwanamuziki ambaye ni zao la Jumba la Vipaji Tanzania ' THT' Estalina Sanga ' Linah ' ameaga rasmi jumba hilo ambapo inadaiwa kwa sasa atakuwa chini ya Kampuni ya No Fake Zone ' NFZ ' inayoendesha shughuli zake nchini Afrika Kusini.

Mwanamuziki ambaye ni zao la Jumba la Vipaji Tanzania ‘THT ' Estalina Sanga ‘Linah ' Akizungumza na Ijumaa msemaji wa kampuni hiyo aliyewahi kushiriki Shindano la Big Brother Africa 2003 , Abergail Brigette Plaatjies ' Abby ' alisema wamemchukuwa Linah ili kuendeleza kipaji chake kimataifa.

"THT imemlea vizuri Linah na kumfikisha hapa alipo sasa sisi kama NFZ tumemchukua ili tuweze kumuingiza zaidi kwenye soko la kimataifa na kwa kuanzia tumeanza kumtengenezea video ya wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la Oleh Tembah, " alisema Abby .
 
mmh ameondoka huko!asipokuwa makini watampoteza jumla coz ukishajitoa wanakuharibia kila kitu.
 
mmh ameondoka huko!asipokuwa makini watampoteza jumla coz ukishajitoa wanakuharibia kila kitu.
Yah ni kweli wanakuthamini ukiwa nao maana kuna kitu wanaingiza kupitia jasho lako, kwa kuwa ametoka lazima wamuharibie.
 
Yah ni kweli wanakuthamini ukiwa nao maana kuna kitu wanaingiza kupitia jasho lako, kwa kuwa ametoka lazima wamuharibie.

Mmh mimi hofu yangu wasije kumbebesha madawa tu linah wetu wakamfanya punda, maana hakuna cha bure mjini apa mtu sio baba yako aku manage bure tu?
 
Wasimfanye kama yule mwingine wa binti Sumari, walimbogozoa kisha hakuna promo wala nini, akarudi nyumbani analia tukamwonea huruma. alafu hao waafrika kusini ndo walijifanya kumpa mkataba Miriam Odemba kipindi bado yuko kigori, walivyokula mzigo wakatosheka, wakamwambia eti kanenepa. Maisha haya ya wasichana wetu, hatari tupu.
Anyway, good lucky Lina Sanga.
 
Hiyo nyimbo aliyotoaa mbona kawaiga mafikizoro lo
 
Back
Top Bottom