Linapokuja suala la filamu, nauheshimu sana Mkoa wa Tanga

Kidedea (chini ya mwanadada Peace), Mambo Hayo (Nyota Ensemble chini ya Bishanga na wenzake) na Kaole yalikuwa makundi matatu tofauti yaliyorusha michezo ITV. Kidedea ndo iliyowaibua akina Jengua, Tabia n.k...
Kuna madogo hawajawahi kuona hii michezo aisee daah enzi hizo michezo mitamu sana kuangalia Mzee Magari na msemo wake wa 'Mahinda Maidota'
Kaole hio
 
Kidedea (chini ya mwanadada Peace), Mambo Hayo (Nyota Ensemble chini ya Bishanga na wenzake) na Kaole yalikuwa makundi matatu tofauti yaliyorusha michezo ITV. Kidedea ndo iliyowaibua akina Jengua, Tabia n.k...
Nimemkumbuka Bishanga Bashaija 😂
 
Tunaomba utuwekee nakala yake hapa na Sisi tuiangalie haujaipandisha YouTube utupe link?
 
Kibuyu ilikua vizuri Sana marehem king majuto aliitendea haki .
 
Kampuni ya kutengeneza filamu ya Whatever Film Productions ya Tanga, ndiyo kampuni namba moja Tanzania nzima. Jamaa wanajitahidi sana
 
Kidedea (chini ya mwanadada Peace), Mambo Hayo (Nyota Ensemble chini ya Bishanga na wenzake) na Kaole yalikuwa makundi matatu tofauti yaliyorusha michezo ITV. Kidedea ndo iliyowaibua akina Jengua, Tabia n.k...
Hey nafahamu yote hayo.

Kuhusu kidedea achilia mbali nakumbuka kama kuliwahi kuwa na tamthiliya yenye jina hilo.

Kidedea kama sikosei alikuwa yupo Mzee Jengua.

Kaole wapo akina Swebe Santana, Nina, Muhogo mchungu, nyamayao, kibakuli, Kanumba,Johari, Nora,Ray Vincent kigosi nk

Mambo hayo bishanga ,Richie Richie ,Waridi nk.
 
Mmm mimi mzee wa busara ndo niliona kali zaid kwa upande wa horror
 
Isee enzi hizo hukosi hii michezo saa tatu usiku jumamosi yaani tv hapo antena za samaki chenga kwa mbali yaani mara inazingua.

Alafu tamthilia za zamani mnakaa familia zima mnaangalia
Nakumbuka michezo km maisha ndani kuna kibakuli na nyama yao, muhogo mchungu bi stara mchepuko hatari sana huko kuna dr. Cheni na sekeseke lake..
Mchezo mwingine ni kidedea unaamshaamsha balaa huyo jegua alikuwa moto fireee kila binti anapita nae mtaani na mwanae pasua kichwa.

Mwingine ni mabo hayo hapo kuna muhaya bishanga na waridi huu sikumbuki vizuri maan ndio nilikuwa naanza kujitambua ila kilikuwa kipindi fulani hivi cha raha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…