Ni ukweli usiopingika kwamba Dar ina watu wengi walioelimika (Educated) na wenye exposure kubwa katika mambo mbalimbali kama elimu, biashara, sanaa, michezo n.k.
Hivyo ni jiji ambalo watu wake wanajielewa sana(simaanishi majiji mengine watu hawajielewi, hapana wanajielewa lakini Dar ni zaidi sana kwa asilimia kubwa kutokana na kuwa na idadi kubwa ya walioelimika na wenye exposure kubwa)
Hivyo watu katika jiji hili la Dar hatufuati mkumbo, kushikiwa akili n.k. tunataka "Utupe sera"
Ni ukweli usiopingika, kwamba JPM amefanya kazi kubwa katika miaka mitano na anastahili kuendeleza kazi kubwa alioianza katika miaka mitano ijayo.
JPM amefanya restructure kubwa katika system ya nchi kwenye sector mbalimbali. Kwa mtu yoyote ambaye ameelimika hatilii shaka kazi alioifanya JPM. Dar na watu wake tunatambua kazi alioifanya JPM katika nchi hii.