Hawa wa DSM wanataka sana HOJA, uwaeleze mambo kwa hoja siyo uwatake wafanye mambo kwa MIHEMUKO. Wa Dar-es-Salaam wana mambo mengi ya kulinganisha hasa inapokuja kwenye masuala ya elimu, miundombinu, mahospitali na mambo mengine mengi ya maendeleo.
Wengi, nje ya jiji la Dar-es-Salaam labda wana kosa uwezo wa kudadavua mambo na hoja za wanaharakati, wapinga maendeleo na vibaraka wao. Kwa mantiki hiyo kuwafanya washabikie kila neno toka kwa wapinzani, ingawa SI KWELI WAKATI WOTE! Ona wananchi na Watanzania katika nchi yote watoavyo hoja za kupinga kauli za akina Lissu, Zitto na wengine kuhusu maendeleo tunayoyaona hapa nchini.
Kila mtu anajua umuhimu wa miundombinu ya reli, barabara, flyovers, ndege, bandari, usafiri wa majini, vivuko n.k. katika ujenzi wa uchumi kuwa HIVYO NI VITENDEA KAZI katika kuharakisha na kuchangamsha biashara (za nje na za ndani), kuharakisha utoaji wa huduma muafaka na mambo mengine kama hayo ambayo wewe na mimi tukiyachangamkia tutanufaika KIUCHUMI, tofauti na dhana na madai potofu kuwa "hayo ni maendeleo ya vitu"! Hawa wachumi wa leo wana mambo ya AJABU SANA, SIJUI VIPI?