Lindi: Bilioni 13.95 kuwaunganisha kwa Daraja Wananchi wa Nanjilinji na Ruangwa

Lindi: Bilioni 13.95 kuwaunganisha kwa Daraja Wananchi wa Nanjilinji na Ruangwa

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Wananchi wa Nanjilinji na Ruangwa wameelezea furaha yao kufuatia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto Nakiu, hatua inayotajwa kuwa suluhisho la kudumu kwa changamoto za usafiri, uchumi na huduma za afya ambazo zimewakumba kwa miaka mingi.
Mradi huo, unaogharimu shilingi bilioni 13.95, utekelezaji wake unaendelea kwa kasi chini ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa maelekezo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukitarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.

Ahmad Kinongo ambaye ni mkazi wa Nanjilinji, ameeleza kuwa, ujenzi wa daraja hilo unarejesha matumaini kwa wananchi waliokuwa wakikumbwa na changamoto kubwa, hasa wagonjwa waliokuwa wakikwama kuvuka mto kufuata matibabu Ruangwa.

Kwa upande wake Rajab Selemani Fungire ametoa pongezi maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa dhamira yake ya kuunganisha wananchi na kuboresha miundombinu ya nchi.

"Kwa miaka mingi, Masika imekuwa adui yetu, bidhaa zinapanda bei na usafiri unakwama. Sasa, kwa uongozi wa Mama Samia, tunaiona nuru mpya," alisema kwa shukrani.
 
Dah! Baada ya miaka 60+ ya uhuru hatimae.
Tutafika naamini, lakini kwa kuchelewa sana.
 
Back
Top Bottom