Lindi: Mabasi ya Saibaba na Baharia yagongana uso kwa uso 7 wapoteza maisha

Lindi: Mabasi ya Saibaba na Baharia yagongana uso kwa uso 7 wapoteza maisha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ajali ya barabarani iliyohusisha gari mbili za abiria, Saibaba iliyokuwa inatoka Nachingwea kwenda Dar na Baharia iliyokuuwa inaelekea Nachingwea. Ajali hii imetokea jana mchana tarehe 05.10.2023 katika eneo la Kiwawa, Mkoani Lindi.

Tunasubiri Taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka

=====

Watu saba wamekufa na wengine 22 wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea katika Kijiji cha Kiwawa kilichopo Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, ikihusisha basi aina ya Scania mali ya kampuni ya Saibaba na basi aina ya Tata, mali ya kampuni ya Baharia.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Pili Mande amesema ajali hiyo imetokea jana jioni, ambapo miongoni mwa waliofariki dunia ni pamoja na dereva aliyekuwa akiendesha basi la kampuni ya Saibaba, Lucas John (59) ambaye ni mkazi wa Arusha pamoja na dereva wa basi la kampuni ya Baharia, Omari Alli Abdalah (49) mkazi wa Dare s salaam.

Amesema miili ya marehemu watano bado haijatambuliwa majina yao mpaka sasa.
1696574515275.png
1696574527711.png
1696574540391.png
1696574551545.png
1696574563874.png
 
Back
Top Bottom