Lindi: Mama amnywesha mwanaye wa mwaka mmoja sumu kwa kushindwa kukaa naye

Lindi: Mama amnywesha mwanaye wa mwaka mmoja sumu kwa kushindwa kukaa naye

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
WATOTO wawili mkoani Lindi wamefariki dunia katika matukio tofauti, likiwamo la mama mzazi kudaiwa kumnywesha sumu ya kuua magugu kutokana na kinachodaiwa kuchukizwa na kitendo cha mkwe wake kukataa kumchukua mjukuu wake huyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka wilayani Nachingwe na Ruangwa yalikotokea matukio hayo huku zikithibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Foka Dinya, matukio ya vifo vya watoto hao wenye umri wa mwaka mmoja kila mmoja, yalitokea mchana wa Machi tano mwaka huu na usiku wa Machi sita mwaka huu.

Kamanda Dinya aliiambia Nipashe jana kuwa mama wa mtoto aliyedaiwa kunyweshwa sumu, ni mkazi wa Kijiji cha Mchichili, Wilaya ya Ruangwa.

Inadaiwa kuwa mauaji hayo yalifanywa na mama huyo ambaye polisi wameficha jina lake, Machi 5 mwaka huu majira ya saa tano usiku baada ya mama mkwe wake kumkatalia kumpokea mjukuu wake kwa maelezo kwamba bado ni mdogo na anahitaji kunyonya maziwa ya mama yake.

"Mtuhumiwa alimchukua mwanawe na kumpeleka kwa bibi yake, lakini bibi alikataa kumpokea kwa vile alikuwa bado ananyonya," alidai Kamanda Dinya katika mazungumzo na Nipashe kuhusu tukio hilo jana.

Alisema uchunguzi wao wa awali umebaini kitendo cha bibi kukataa kumchukua mjukuu wake, kilisababisha mtuhumiwa ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano, kuchukua uamuzi wa kumuua mwanawe ilipofika majira ya saa tano usiku.

Kaimu Kamanda huyo alidai kuwa mtuhumiwa alichukua sumu ya kuulia magugu na kumnywesha mtoto huyo na kuukatisha uhai wake.
Kamanda Dinya alisema mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu shtaka linalomkabili baada ya kukamilika taratibu zote, ikiwa ni pamoja na upelelezi.

Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinalitaka Jeshi la Polisi ama kumfikisha mahakamani au kumwachia huru mshtakiwa ndani ya saa 24 tangu kukamatwa kwake isipokuwa kwa makosa yanayohusiana na adhabu ya kifo.

Katika tukio la pili, kwenye Kata ya Ugawaji, Tarafa ya Nambambo, Wilaya ya Nachingwea (jina halijatajwa), amefariki dunia kutokana na kinachodaiwa kutumbukia kisimani alipokuwa akicheza na wenzake.

Kamanda Dinya alisema kisima hicho chenye urefu wa futi 12, kilikuwa kimejaa maji na mwili wake ulipoopolewa, ulifanyiwa uchunguzi na wataalamu wa afya kisha kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi.

NIPASHE
 
Kuna member mmoja humu huitetea sana Kusini dhidi ya mauwaji ya kifamilia yaliyoibuka kwa kasi nchini. Haya mavitu hayachagui eneo; ni suala la muda tu litafanywa tukio litawaacha midomo wazi.
 
Kuna member mmoja humu huitetea sana Kusini dhidi ya mauwaji ya kifamilia yaliyoibuka kwa kasi nchini. Haya mavitu hayachagui eneo; ni suala la muda tu litafanywa tukio litawaacha midomo wazi.
Ila hauwezi fananisha na kaskazini
 
Huyu atakuwa alipata mwanaume wa kumuoa so akaona mtoto atamletea vikwazo, N.B sijasema single mothers.
 
Huyo mama akili zake hazina utofauti na Zile za Comedian Zerensky wa Ukraine
 
Hizi habari za kuuana ni lazima muwe mnaziandika? Maana imekua ndio trend sasa ad kero 😡
 
Back
Top Bottom