Pre GE2025 Lindi: Mbunge wa Viti Maalum achangia bati 90 ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Nachingwea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Tarehe 3 Machi 2025 Maimuna Pathan, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi, amekabidhi bati 90 kuunga mkono juhudi za ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Nachingwea. Bati hizi ni sehemu ya michango ya Pathan katika kuendeleza maendeleo ya Wilaya ya Nachingwea na Mkoa wa Lindi kwa ujumla.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pathan amesema kuwa ni furaha yake kuona wananchi wakishirikiana katika kujenga jamii bora, na alisisitiza kuwa ataendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwa kutoa mchango kwa miradi muhimu, ikiwemo hiyo ya ujenzi wa nyumba za watumishi ndani ya Chama.

"Ujenzi wa nyumba hii ni muhimu sana kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya Wilaya yetu. dhamira ya dhati ya Uwt Wilaya naiunga Mkono alisema Pathan.

Aidha Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nachingwea, Salima Chilima, ametoa shukrani za dhati kwa Mhe. Pathan kwa mchango wake, akisema kuwa michango yake inatia nguvu na kuongeza ari ya kujitolea kwa viongozi wa UWT na jamii kwa ujumla.

"Pathan, tunakushukuru kwa moyo wako wa kujitolea na kujali maendeleo ya Wilaya yetu. Hii ni ishara ya wazi ya ushirikiano wa kweli kati ya viongozi na wananchi, na tunakuahidi kuwa tutadumisha juhudi zako katika kuleta maendeleo," alisema Chilima.

Mhe. Pathan ameendelea kuonyesha uongozi wa mfano katika Mkoa wa Lindi, akijitahidi kuwa kielelezo cha juhudi na kujitolea kwa maslahi ya umma, na sasa wananchi wa Nachingwea wana furaha ya kuwa na mtumishi wa umma anayejali na kuhamasisha maendeleo ya mkoa mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…