mud-oil-chafu
JF-Expert Member
- Dec 27, 2020
- 587
- 954
Aàah nmekupata mkuuTujipange
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aàah nmekupata mkuuTujipange
Dah! Nimecheka hatari 😂😂😂😂😂wenzetu wanakuwaga na vimbunga vina majina romantic kabisa mfano catrina ila sisi eti JOBO jamaan JOBO kweli this is unfair
Ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam umetoa tahadhari ya kiusalama kwa wafanyikazi wake walioko nchini Tanzania kuhusu hatari ya Kimbunga Jobo kinachoeleka katika pwani ya nchi hiyo na kitaufikia pia mji wa Dar salaam .
Kupitia tahadhari kwa wafanyikazi wa ubalozi wake , afisa anayesimamia usalama Robert Gousie amesema kimbunga hicho kinatazamiwa kutua Tanzania kufikia tarehe 25 Aprili.
Amesema hakuna uhakika kuhusu ukubwa wa athari zake na mengi bado hayajulikani kwnai kuna vingi vinavyoweza kubadilika katika siku zijazo .
Taarrifa yake imeeleza kwamba miongoni mwa hatari kusababishwa na kimbunga hicho ni kuwepo upepo mkali ,mawimbi ,mafuriko na mvua kubwa . Mkuu huyo wa usalama amewashauri wafanyikazi wa ubalozi wa Marekani na watu katika sehemu zitakazoathiriwa kuchukua hatua zifuatazo kimbunga hicho kinapokaribia;
Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutua Tanzania tangu mwaka 1952.
- Kusalia nyumbani ili kuepuka hatari
- Kutosafiri wakati huu kwani mvua kubwa na upepo mkali zinaweza kuziharibu barabara
- Kuhakikisha wana chakula na maji ya kutosha katika nyumba zao ,na kuwa tayari kusalia kwenye makazi yao iwapo mvua na upepo vitazidi
- Kuingiza ndani vifaa vilivyo nje ambavyo vinaweza kuwa hatari vikibebwa na upepo
- Kuhakikisha magari yao yana mafuta
- Kuhakikisha simu zao zina moto na kujitayarisha kwa safari ya dharura endapo hali itabadilika na kufuatilia taarifa kuhusu kinachofanyika kupitia vyombo vya habari
Ripoti zilziotolewa jana zilisema kimbunga hicho kilionekana kaskazini mwa Madagascar kikiwa na kasi ya kilomita 83 kwa saa.
Utabiri ulionyesha kuwa kimbunga hicho kilipiata Ushelisheli Aprili tarehe 22 kikiwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa na kinatazamiwa kutua Tanzania Aprili 24 au 25.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadahrisha kuwa kimbunga hicho cha Bahari ya Hindi kinaweza kusababisha upepo mkali na mawimbi makubwa baharini katika maeneo ya Lindi na Mtwara. Aidha kuna uwezekano wa kutokea mafuriko katika maeneo athirika.
TMA imesema itaendelea kufuatilia kimbunga Jobo na kuwapasha wananchi habari kuhusu tahadhari zinazopasa kuchukuliwa.