Lindi: TAKUKURU yabaini kasoro miradi ya Tsh 928,340,557

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
LINDI: TAKUKURU YABAINI KASORO MIRADI YA TSH 928,340,557

Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi imebaini kasoro katika miradi miwili yenye thamani ya shilingi 928,340,557 wakati wa mchakato wa kufuatilia miradi mkoani hapo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2022.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi, Abnery Mganga amesema kasoro zilizobainika ni ucheleweshwaji wa miradi kumalizika ndani ya muda, ikiwa ni miradi miwili kati ya 18 iliyofuatiliwa.

Amesema TAKUKURU ilifuatilia jumla ya miradi 18 yenye thamani ya Shilingi 3,744,489,057, ambapo miradi 16 iliyosalia yenye thamani ya Tsh. 2,774,489,057 haikukutwa na kasoro










 
Hizi ripoti bana! Nyiiiiiiiiiiingi!
Sijawahi kuona mrejesho hata mmoja!!
Au mambo yote yanaishia kwa DPP?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…