Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Zaidi ya wanachama 50 wa Chama cha ACT Wazalendo wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM), wakisema walichojifunza upinzani ni ukaidi na vurugu na sio kufanya mambo yenye manufaa kwa wananchi.
Wanachama hao wamepokewa leo Aprili 13,2025 na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Lindi Mjini mkoani Lindi, akiendelea na ziara yake kutembelea mikoa ya Lindi na Mtwara kwa siku 10.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake, aliyewahi kuwa Diwani na Mwenyekiti kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Said Kitunguli, amesema awali alikuwa mwanachama wa CCM na mwaka 2008 alihamia CUF, lakini utekelezaji wa Ilani ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ndio sababu kubwa ya kumfanya arudi CCM.
Wanachama hao wamepokewa na Makalla wakati akitambulisha wageni alioambatana nao katika ziara hiyo ambao ni aliyewahi kuwa Mbunge wa Iringa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa.
Wengine ni aliyewahi kuwa Mkuu wa Mawasiliano wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya na Rashid Sepanga, ambaye alihamia CCM Novemba, mwaka jana na kusema kuwa wanachama hao wapya ni zawadi kwa CCM
Source: Nipashe