Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi
Majambazi wawili ambao majina yao hayajafahamika wameuawa na wananchi wilayani Kilwa Mkoani Lindi, baada ya kuvamia duka la mfanyabiashara mmoja na kupora fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 1.2.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 5, 2022, majira ya saa 2:00 usiku katika Kijiji cha Kisongo Pande wilayani Kilwa mkoani humo.
"Watu hawa walikuwa wanne, wawili waliingia ndani na wawili walibaki nje na kupiga risasi juu ili kuwatisha wananchi na yule aliyevamiwa walioingia ndani walipora milioni 1.2, kutokana na Polisi Kata na ulinzi shirikishi wananchi waliweza kujikusanya na kuwadhibiti majambazi hao," amesema Kamanda Kitinkwi.