mrdocumentor
Member
- Nov 27, 2021
- 45
- 56
Lindi ni miongoni mwao mikoa inayopatikana ukanda wa kusini pamoja na mkoa wa Mtwara na Ruvuma, katika mkoa wa Lindi yanapatikana makabila tofauti tofauti lakini ukiniuliza wenyeji wa Lindi ni kabila gani? Jibu rahisi ni Wamwera. Vipo vitu vingi sana vya kujivunia kutoka Lindi Ikiwemo uwepo wa bahari, magofu ya kale ya kilwa, gesi ya songosongo bila kusahau kuwa Lindi ndio mkoa ambao waziri mkuu wa sasa ametokea, pia usisahau kuwa Lindi Redio yetu kubwa ni Mashujaa fm radio. Kwa uchache rizika na huo wasifu mdogo wa mkoa huu mzuri ulioysahaulika.
Jambo kubwa ambalo tumekuwa tukijivunia kwa muda mrefu kwa sasa kutoka katika mkoa huu ni AMANI, Kwa ujumla Tanzania amani ndio amana yetu isiopotea lakini Lindi haikuwa na amani tu kama Sehemu ya Tanzania bali Lindi ilikuwa na amani hata kwa mtu mmoja mmoja suala ambalo kwa sasa limeanza kupotea au lipo katika hatari kubwa ya kupotea.
Siku moja wakati napita katika mtandao maarufu kwa vijana Instagram, nkapata taarifa kuwa Kuna kijana amejikata uume!! Usishangae!! ndio ni uume huo huo unaoujua wewe. Sababu ya kufanya hivyo baadae ilionekana kuwa mhusika alishawahi kuwa na tatizo la afya ya akili.
Wakati nasema inatosha sasa! Mara kijana mmoja kanitag kwenye Comment ya post ambayo heading ya taarifa ilisomeka kwa ujumbe usemao "Ajinyonga akidai watu wanamvuruga" ilikuwa Lindi Pia.
Nataka kusema nini? Lindi haya sio mambo yetu, turudi katika asili yetu kwa jitihada zetu na kwa kuomba pia.
Lindi tumezoea kusikia taarifa za Bei ya ufuta na korosho kupanda na nyingine nyingi nzuri na za kufurahisha sio hizi zinazo trend kwa sasa.
#Lindiicon