Line 1 wa "John Bocco" kafikafikaje kuchezesha Ligi Kuu?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Jana kuna mtu anaitwa JAPHET KASILIRWA kutoka Rukwa, alikuwa mwamuzi msaidizi namba 1 Uwanja wa Taifa mechi ya Simba V Coastal.

Kayafanya mambo anayajua yeye pekeyake sababu binafsi nimefanya uchunguzi mdogo juu ya maamuzi yake ya offside zile lakini amekosa uungwaji mkono. Wote wanamuona hajui sheria namba 11 kwahiyo utafsiri wake wa sheria ni mdogo.

My take!
Huyu mwamuz msaidizii asiyejua sheria namba 11 inayohusiana na Kuotea (Offside) amefikaje hapo alipo? Offside ina amuliwa na mwamuzi msaidizi pekee na mwamuzi wa kati kazi yake ni kupuliza filimbi tu.

Kama kuna sheria mwamuzi msaidizi anapaswa kuijua vema mbele ya zote basi ni hii ya kuotea, ambayo yeye ndiye mwamuzi wake wa moja kwa moja. Sasa unampataje Kasilirwa kuchezesha Ligi Kuu huku uwezo wake juu ya hii sheria ukiwa ule wa jana? Unagundua kwamba kuna ujinga mahali umefanyika.

Waswahili husema "Ukiona Kobe mtini, ujue amepandishwa". Hii maana yake ni kwamba Kobe hawezi kupanda mti lazima apewe msaada, anayempandisha anajua kwanini amemuweka hapo mtini. Huyu mwamuzi amefikaje hapo tena akapewa na mechi ya 'Sebuleni'?
 
Minamashaka hakuwa timamu kwa siku ya jana, ama alikua amelewa, kavuta ganja mganjuko au alikua anamatatizo ya kiakili.
 
Huyo Mshika Kibendera aliboa sana. Magoli 3 aliwanyima Simba kwa kudhani wameotea. Ikibidi next time aondolewe kabisa.
 
Mimi nafikiri huyo mwamuzi ni mbumbu wa sheria ya kuotea na TFF wanapaswa kumfungia, kumpiga faini na kumshushwa daraja kabisa akachezeshe ligi za mikoa na pia arudi darasani kwa faida yake huko mbeleni.

Najaribu kufikiria ile ingekuwa mechi kati ya Simba na Yanga, Simba na Azam au Yanga na Azam si ingekuwa balaa pale Taifa. TFF, bodi ya ligi na kamati ya waamuzi wawe makini sana na waamuzi kama hao kwani ipo siku watakuja kuleta maafa uwanjani .

Kwake yeye washambuliaji wa Simba wakiwa na mpira mbele ya goli la Coastal bila kujali aliye na mpira hakuwa offside na wengine hawakuingilia mchezo yeye alikuwa anainua kibendera chake.

Na ni mbumbu kweli wa sheria ya kuotea kwani kafanya kosa hilo hilo zaidi ya mara kumi ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza chote.
 
Yote ni sawa ila Kiswahili sanifu ni mwamuzi. Kuna mambo ya kanuni za lugha hapa, ua zikiambatana huzalisha sauti 'w'. Ni kama ilivyo kwa mualimu=mwalimu na maneno mengine mengi.
Hivi ni Mwamuzi au Muamuzi?

Msaada kidogo wakuu!!
 
Hata ligi daraja la kwanza hawatoi maamuzi kama yale
 
Yote ni sawa ila Kiswahili sanifu ni mwamuzi. Kuna mambo ya kanuni za lugha hapa, ua zikiambatana huzalisha sauti 'w'. Ni kama ilivyo kwa mualimu=mwalimu na maneno mengine mengi.
Sawa Mkuu,nashukuru sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…