Linex aapa kutofanya kazi tena na Adam Juma

Anachosema Linex ni sawa AJ alimfanyia uhuni maana ukiangalia quality kubwa ya video ya Salima ni 480p ambayo ni low ukizngatia sahv quality kubwa ya video ni 1080HD pixels kwa video nyingi zinazotoka.
Kwaio kukataliwa na Tv Stations nyingine ni sawa maana wanataka kurusha kitu quality kiwafikie watazamani na ukizingatia sahv tv ziko katka technology kubwa big screen wides Tv kwa 480p haiwez kufit kwenye Tv ya Inch 55 ukaenjoy picture lazma vizuri lazma iwe 1080HD.
Wema kwa Ubaya ilikua na good quality kushinda Salima.

 
Jamaa anakosa kujitambua....Dah mbaya sana kwa msanii.
 
Watu mnaziongelea hizi mil 40 au 50 kirahisi rahisi tu. Ngoja niwaache maana wabongo kwa kujipandisha hamjambo
 
hivi kuna video aliyoshoot adam juma ikachezwa MTV? na hadi sasa kashashoot videos 600+ huyu adam nae ni jipu.tena sio jipu ni busha kabisa!
 
AJ sio director mzuri kabisa.Kwa bongo HASCANA ndio jembe, AJ alianza kitambo sana toka yuko Visual Lab, sema either it seems hataki kukua au ana pride sana. Yeye angejitengenezea jina kwa kutengeneza video kali, ila ukianga ile ya chegge na temba, unaona kabisa camera inacheza, nyimbo haina script, watu wako wako tu, sasa watu wanamkimbia, Angalia chupa ya nasema nawe ya chibu, dogo kaanza juzi juzi lakini katengeneza bonge la video.
AJ kutwa kulalamika anapewa hela ndogo. C ukataeee
 
Duh ndugu naona umedadavua kitaalam watu wengi hawawezi kukusoma, ila muhusika jibu analo hapo
 
Ukiachaga ushabiki una point balaa.
 
Walisema wahenga "penye nia pana njia" huyu ndugu hana nia ndio maana hata njia haoni.

Nakumbuka Nay baada ya kutoridhishwa na video alirekodi upya na kuachana na ile ya awali, na sidhani kama mpaka leo hii Nay anaendelea kulia kuhusu ile video....kwa nini? kwa sababu Nay alikuwa na nia hivyo akaiona njia..aka move on.

Jamaa analia kila siku kuhusu hiyo video moja as if ndio ngoma pekee aliyonayo mpaka sasa.

Hebu akae chini apime kama hayo malalamiko yana/yatamsaidia kiasi gani kimuziki?

Ngoma kama ni ya kupendwa itapendwa tu, hata kama video yake itakuwa haitazamiki.

Kuna wimbo wa eddy kenzo wa "Maria rosa" video sio official ina comedians wawili wanacheza mwanzo mpaka mwisho lakini mpaka sasa ina view mil 4, na ipo official video yake........sasa kinachovuta views pale ni video au audio?...mimi sijui.

Ngoma kali ni kali tu, ikikubalika you tube na kwingine sidhani kama tv zitaakuumiza kichwa.
 
Wabongo kwa visingizio hawajambo! Ml.5 unataka video ikamate afrika? Mondy na Kiba wataendelea kuwa masupa staa wa bongo mpaka wakatae wenyewe.
 
Haka kajamaa inabidi kawe na akiba ya maneno..Haya sio maneno ya kuongea kwenye media..Anajiharibia
jamaa nilimsikia, aisee nildharau kweli, sijui alienda studio akiwa amevuta? yaani jamaa kamuumbua jamaa hadi dah, aige mfano kwa akina diamond aisee, jamaa mimi sio shabiki wa kazi zake lakini ana nidhamu sana huwezi kusikia amem diss mtu live hata kama ameulizwa maswali ya kimtego kama ya salama
 
Umeona ee, mfano mzuri ni ule wimbo wa 20% 'Tamaa mbaya', ile video Kama imechukuliwa na simu ila ilimuweka juu Sana kutokana na uzuri wa audio, so asimsingizie Adam kufeli kwa salima
 
Adam Juma ni legendary wa industry ya video kwenye
Bongo Flava.Alikuwepo toka kwenye hatua za kwanza
kabisa za hii kitu na haiwezi kukuacha na mshangao
ukijua kuwa ‘jamaa’ ndio video director ambaye jina
lake limetokea kwenye video nyingi kuliko mwingine
yoyote.

Salima ni wimbo mzuri ambao ulihitaji video nzuri zaidi
ya video ambayo tunaiona leo hii.

Mwanzo hatukujua nani ni tatizo tukawa hatujui nani
anastahili kubeba lawama kwa ubovu wa video ile.Ila
Linex amekuwa wazi kwa kudondosha lawama nyingi
kwa Adam Juma kuwa amemuangusha mno kwa
kuifanya video yake kuwa ya kawaida.

Adam naye hakuwa mpole kwa kuweka wazi kuwa
Sunday Mjeda hakuwa amewekeza hela za kutosha
ndio maana video ikawa ya kawaida.

Kauli ya Adam inakufanya ushtuke inakuaje kwa
msanii A-List kama Linex kuwa “Mbahili” kama kweli
anataka kupiga hatua kwenda mbele na sio kurudi
nyuma? Tunasikia kila leo wenzake wanavyopishana
viwanja vya ndege kwenda kwa Godfather,Clarence
Peters,Moe Mussa,Kelvin Bosco na wengine wengi
kule Kenya kutafuta ubora wa video zao kwanini isiwe
kwake yeye?

Sidhani kama Adam Juma ni tatizo la kukwama kwa
video hii kila siku naiangalia video ya Rich Mavoko
“Pacha wangu” ni moja kati ya video bora kutoka kwa
Adam Juma na Rich Mavoko aliweka wazi kuwa
aliwekeza zaidi ya shilingi milioni 10 za Tanzania
kupata video yenye ubora ule.

Utapata wapi video yenye ubora ya kuchezwa MTV,
Trace, Channel O au Sound City kwa kuwekeza million
3 za kitanzania?!

Ni nani aliruhusu video iende hewani kama ikiwa haina
ubora unaotakiwa!?

Iko wazi video director akishamaliza kazi yake
anampa msanii video yake na kama ikiwa ina
mapungufu msanii anairudisha tena kwa director ili
irekebishwe au kufutwa kabisa na kuanza upya
kushoot! Je Linex na team yake hawakuona
mapungufu ya ile video mpaka video ikiwa ishatoka?!

Ni kweli Adam Juma ana mapungufu yake kama
binadamu wa kawaida ila kwa hili la Linex hapana
hastahili lawama hizi kumlaumu ni kumuonea. Ikiwa
kukodi camera nzuri kama zile za Godfather kwa siku
moja ni shilingi milioni 1.5 hadi 2 nje ya hela
utakayomlipa kwa ku-direct video yako, utawezaje
kupata video nzuri kwa milioni 3 nje ya kukodi camera
ya kisasa?!
 
Qual
Quality ya video kwenye youtube haina maana kuwa hiyo video haikutengenezwa kwenye quality ya hd, inawezekana waliupload kwa quality ndogo kupunguza size ya file. Ila wakipeleka kwenye TV stations wanapeleka full quality.

Pamoja na hayo video sio nzuri na wimbo sio mzuri kihivyo.

Lawama hapa wagawane 5mil ni ndogo sana lakini video pia imekosa basics kabisa za kuifanya iwe watchable.
 
Kuna video zina mpaka Mb 40 lkn ni 1080HD kwaio sidhani kama waliUpload 480p ili kupunguza ukubwa wa file hapana. nadhani linex alikabidhiwa video yake ikiwa 480p kama final product course kama angepewa 1080p sio mjinga aweke 480p YouTube.
 
mzaramo mi naona Linex amepanic baada ya kuona wimbo haukufanya vizuri kama alivyotarajia, malalamiko yake hayamake sense maana Kama ulivyosema ilitakiwa ambane AJ kabla video haijatoka baada ya kuona mapungufu, kumsema vibaya baada ya kuona haikufanya vizuri sio sawa. Halafu ye mwenyewe kasema jamaa alimpa na ofa ya kushoot video nyingine bure so anacholia nini?
 
Kuna video zina mpaka Mb 40 lkn ni 1080HD kwaio sidhani kama waliUpload 480p ili kupunguza ukubwa wa file hapana. nadhani linex alikabidhiwa video yake ikiwa 480p kama final product course kama angepewa 1080p sio mjinga aweke 480p YouTube.
Bundle baba, Linex na bangi zake akaamua aweke 480p haha!
 
Bundle baba, Linex na bangi zake akaamua aweke 480p haha!
Haha inawezekana maana nishawah kumuona mitaa flani ya Mbezi beach dah sikumuelewa kabisa nikasema labda ni stress za mziki..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…