Nakuunga mkono, no matter how good one, akikaa muda mrefu, anachosha, hivyo mabadiliko ni muhimu from time to time, CCM kina utaratibu mzuri wa miaka 10, anakuja mwingine, naomba kukuuliza, ukiondoa CCM, nani mwingine wa kutuletea maendeleo ambaye ni mzalendo, na mwenye sera chanya zenye maslah mapana ya Taifa, ili tumpe Ikulu yetu?.
P
Sidhani kwamba Kweli Tanzania hatuna watu wakuweza kuliongoza Taifa hili vizuri zaidi ya Wafanyavyo CCM. Naamini hata Nyerere alipostaafu wapo waliodhani sasa tunaelekea kuzimu kama taifa, lakini tizama bado tupo. Vivyo hivyo wewe unadhana hakuna awezaye zaidi ya ccm, mi naamini hilo linawezekana.
Utawala siyo chama ni watu, Imagine ccm wavurugane isambaratike unadhani Tanzania itazama? Taifa litabaki na wapo watu wataliongoza, na unaweza kushangaa labda wataongoza vyema zaidi.
Kuhusu vyama, Ni CHADEMA pekee ndio wanaweza unaweza usiwaone lakini wako wengi sana na wenye uwezo mzuri pia.
Tatizo ni mifumo iliyowekwa na CCM. Tizama sasa hivi wapinzani wanaiomba CCM iondoe sheria na utaratibu unaoifanya iendelee kuwepo madarakani. Yani CCM iruhusu kuondolewa madarakani, kitu ninachamini hakitawezekana. CCM hawatokubali, zitapigwa danadana kutwa kucha lakini haitatokea.
Ukweli ni kwamba CCM ikiruhusu matakwa ya wapinzani juu ya katiba, na CCM wakayaheshimu mabadiriko hayo, nadhnai wataondoka mapema sana. Lakini kwasasa hicho kitu hakipo.
Hivyo Naweza kusema nakubaliana na wewe hakuna wa kuing'oa ccm madarakani kwa mazingira ya sasa.
Solution ya Tatizo unaloliona ni Mifumo ccm iliyojiwekea, na hilo ni tatizo kubwa kwa wanao ota kuoondoa ccm madarakani.
Wanasema "if you don't completely understand the magnitude of the problem, you won't fully appreciate the incedible power of the solution" People need to understand the problem first.