Lini tutakuwa Nchi moja, Serikali Moja? Jamhuri ya Tanzania isiwepo kabisa ile Muungano

Lini tutakuwa Nchi moja, Serikali Moja? Jamhuri ya Tanzania isiwepo kabisa ile Muungano

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Tunahangaika sana mara kero mara mauaji mara kulazimishana mtafaruku mkubwa sana ,nahisi ni bora sasa iamuliwe tu na Wabunge tunao wengi sana wakutosha na ziada,tuondoe lile utata Jamhuri ya Muungano liwepo jina zuri la Jamhuri ya Watu wa Tanzania.

Tunaondoa Baraza la Wawakilishi, tunaondoa Serikali ya Mapinduzi tunaondoa vikosi visivyo na kichwa wala miguu wenyewe wanaviita Vikosi vya SMZ muajiriwa atakuwa na hiari yake kuendelea kama muajiriwa wa JWTZ vinginevyo akae nyumbani na kuendelea uraiani na wale JKU wanakuwa JKT.

Itakuwa hakuna tena mambo ya kero zisizokwisha wala chuki za huyu mpemba huyu muunguja ,inawezekana kabisa kwani huu ndio wakati muafaka kabisa ,kuepuka lawama zisizo kwisha.

Ni rai tu naiona inamuelekeo mwema sana.
 
Jambo jema natamani tuungane na ndugu zetu wa damu, utakuwa mfano bora kwa Africa.
 
1. Nenda China, UK, Kenya hata Canada. Ndugu zetu Wanzibar hawajitambulishi km Watanzania. Nilisema na kijana mmoja wa Kipemba Ubeligiji licha ya kutumia passport ya Tanzania lakini alikuwa anajitambulisha nchi yake ni Zanzibar na siyo Tanzania. Kuundoa ubara na uvisiwani dawa ni kuwa na serikali 1 tu.

2. Zanzibar ina population ya 1.6 millions, Tanganyika ina millioni 60.

Licha ya kuwa Zanzibar ina 1.6 millions eti inataka usawa na Tanzania wakati hata kwa mambo yasiyo ya Muungano.

Mtanzania akimaliza form six hawezi pata mkopo wa elimu ya juu Zanzibar but wa Zanzibar wana uwezo wa kupata Tanzania bara au Zanzibar. Hakuna balance kwa bara. Leo tunawaacha mamia ya wa Tanzania bara wanafunzi kuwapa mkopo kwa ajili ya watoto wa Zanzibar.



3. Suala la Ardhi. Suala la Ardhi siyo Muungano' but Wazanzbar wananunua Ardhi Tanzania bara eti sisi Wabara haturubusiwi kununua ardhi Zanzibar. Wtf.

Wazanzibar wanaweza kuja kugombea udiwani au ubunge huku bara Mf. Azan mbunge mstaafu wa kinondoni ni Mpemba! Mbara hawezi pata nafasi Zanzibar ni kazi sana kwa ubaguzi wao huwezi pata.

4. Bado kuna uhasama mkubwa sana kati ya Ugunja na Pemba. Ili kuundoa huo lazma tuwe na serikali 1 strong Zanzibar uwe mkoa kama Simiu. Tanganyika ni silent giant: tunaitaka na sisi Tanganyika.

Kwa muhstari huo juu Nakuomba Mh. Rais Magufuli tunaomba mchakato mdogo wa mabadiliko ya katiba kuhusu Muungano. Tunataka bunge la February liondoe serikali 2. Ibakia serikali ya Tanzania tu. Muungano ni gharaama sana.
 
Mmeanza hivyo, MaCCM mna roho mbaya sana.

Mauaji yote mnayo fanya Zanzibar, lengo ni kupora nchi ya wa Zanzibar?!

Kwa nini msiwaache huru na nchi yao, waamue kama wanataka kuwa sehemu ya hiyo Tanzania ya WAUAJI na WATEKAJI.
 
Chini ya hawa vichaa wa CCM, wenzako wanahesabu zao tofauti na tunazozijua sisi, wao serikali ya Tanganyika, Zanzibar na muungano wanakwambia ni serikali mbili hizo. Yaani 1+1+1=2. Hizo ndio hesabu za wanaCCM ndugu majiniasi wa dunia.
 
Naunga mkono hoja, shida ni hao wahafidhina wa mapinduzi matukufu ya Z'bar.
 
Jambo jema natamani tuungane na ndugu zetu wa damu, utakuwa mfano bora kwa Africa.
Itapunguza gharama pia. Baraza la mawaziri linakuwa moja (obviously, dogo), wabunge pia, na Mkuu wa Nchi mmoja na waandamizi wake. Good idea.
 
Kwani aliekwambia kuna serikali zaidi ya nyingi nani, serikali ni moja ya Tanzania ,sisi wadau wa siasa tunahesabu kama Zanzibar ni jimbo au state au mkoa unaojitegemea, wambieni vilaza wenzenu wachape kazi ili mikoa yao ijitegemee hata kuweza kuwasomesha watoto wao nchi za nje, bila ya Zanzibar sisi CCM tusingelikuwepo, hivi ilivyo inapendeza sana, wakuu wa mikoa ichape kazi ili nayo iwe kama Zanzibar kwa maana nyigine ijitegemee.
 
Kwani aliekwambia kuna serikali zaidi ya nyingi nani, serikali ni moja ya Tanzania ,sisi wadau wa siasa tunahesabu kama Zanzibar ni jimbo au state au mkoa unaojitegemea, wambieni vilaza wenzenu wachape kazi ili mikoa yao ijitegemee hata kuweza kuwasomesha watoto wao nchi za nje, bila ya Zanzibar sisi CCM tusingelikuwepo, hivi ilivyo inapendeza sana, wakuu wa mikoa ichape kazi ili nayo iwe kama Zanzibar kwa maana nyigine ijitegemee.

HUNA HOJA MKUU
 
Hesabu za maccm za ajabu sana serikali ya Tanganyika , Zanzibar na serikali ya muungano jumla ni tatu , hesabu za maccm sasa 1+1+1=2 , CCM majiniasi wa dunia nzima .
 
Muungano umewapa waunguja na wapemba ardhi popote Tanzania. Nawaza vile muungano ukifa watatuachia kila kitu warudi kuanza A

Ngoja wale wa majimbo waje☺☺☺
 
Kama haujui Kuna serikali mbili.ya TANGANYIKA na Zanzibar.
Hilo neno Tanzania ni geresha tu..
 
Kwani aliekwambia kuna serikali zaidi ya nyingi nani, serikali ni moja ya Tanzania ,sisi wadau wa siasa tunahesabu kama Zanzibar ni jimbo au state au mkoa unaojitegemea,wambieni vilaza wenzenu wachape kazi ili mikoa yao ijitegemee hata kuweza kuwasomesha watoto wao nchi za nje,bila ya Zanzibar sisi CCM tusingelikuwepo,hivi ilivyo inapendeza sana,wakuu wa mikoa ichape kazi ili nayo iwe kama Zanzibar kwa maana nyigine ijitegemee.
Umeropoka bila kufikiri boss.
 
Back
Top Bottom