" Ipo siku" na kauli zingine kama "we ngoja tu", "utanitambua siku moja" n.k. Nikauli zinazoashiria kuporomoka kwa hisia juu ya jambo fulani. Bila shaka unakumbuka kile kisa cha sungura na ndizi mbivu. Alianza kwa mbwembwe nyingi akizirukia na kuamini atazifikia. kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo alivyozidi kuporomoka katika hisia zake juu ya ndizi. Mwisho kabisa alipotambua kwamba hawezi kuzifikai akasema " sizitaki mbichi hizi"
Awali aliziona mbivu, baada ya kushindwa kuzipata akapoteza hamu na kutoa kauli ya kushindwa akiwa ameporomoka kihisia akatoa hiyo kauli. Kisa hakikuendelea, lakini kingendelea labda angefikia hatua ya kulia na hata kutoa machozi.
Wewe baada ya kukutana na tatizo hilo uliangalia " a tip of the ice-berg" ukakivamia kama Titanic ukiamini utafanikiwa kukisogeza kumbe chini yake kuna tatizo kubwa sana ambalo huna budi kuliangalia. " Ipo siku" ni kauli inayo onyesha hisia uliyonayo juu ya mwenza wako, na hata akipona tatizo lake si ajabu likahamia kwako. kwani tayari umefikia ile hali ya kutaka kuadhibu, kutia maumivu ili ufanikishe mahitaji yako bila kujali anaye toa huduma hiyo.
Pole sana Mkulu, inawezekana tatizo likawa si la mkeo bali ni lako na lina jionyesha kwa mkeo. Mwaka 2007 wakati nampeleka mke wangu kujifingua baada yakutoka nchini Kenya nilikokuwa kikazi. Hakika nilikuwa nimechoka sana kwani nilitumia usafiri wa basi. Ile nafika nyumbani tu namkuta mke wangu ananisubiri, nilichofanya ni kubadili nguo tu na kumpeleka hospitali. Tunafika pale Sinza, manesi wanasema presha ya mke wangu iko juu. Kwa sababu ninauelewa wa maumbile ya kihisia na kiakili ya binadamu, nilipinga hilo. Mke wangu hakuwa na historia hiyo, ila mimi ninayo. Nikatoa nje nikasimama chini ya mti na kuhesbu mapigo yangu ya moyo, ukweli ni kwamba presha yangu ndo ilikuwa juu. Nikaanza zoezi ya kuishusah nilipojiridhisha nikaludi ndani na kushauri wampime tena mke wangu kwani inwezekana walikosea........ Aaaa walistaajabu, saa tatu kasorobo usiku ule nikapata binti mwingine. Mambo ya maumbile ni mazito. Tafuta suluhisho kauli za NAMNA HIYO HAZITIBU KITU