Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Ukiniuliza kama Tanzania ina kiongozi, nitajibu kuwa ina rais lakini si kiongozi. Ukiuliza kama Tanzania ina sera, nitakujibu kuwa ipo sera ya uchawa.
Ukiuliza, kiuchumi Tanzania inaongozwa na nini, nitakujibu kuwa sera yake ni ya shamba la bibi ambapo wezi huja na kugema watakavyo.
Ukiuliza kama Tanzania ni salama, nitakushauri ufanye utafiti na kuassess utekaji na kuporomoka kwa majengo.
Ukiuiza kama Tanzania ina future, nitakujibu kuwa hata past haina. Kama mwanafalsafa, nawaza tu.
Ukiuliza kama serikali inakusanya kodi na kuzitumia vizuri, nitakujibu kuwa inawakamua maskini na kuwapa matajiri wakwepa kodi na wapiga dili wanaoshirikiana na wanasiasa mafisi.
Ukiniuliza kama Tanzania ni kisiwa cha amani, nitakujibu kuwa ni kisiwa cha vurugu kinachongoja kulipuka.
Kwa wananchi wanavyoteseka huku watawala wakitanua, Tanzania inaweza kuzidiwa na hata Somalia.
Je, ni lini watanzania wataamka na kusema katu kuwa inatosha?