- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Lionel Messi ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Argentina, anayetambulika kama mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya mchezo huo. Alizaliwa Juni 24, 1987, na amechezea klabu ya FC Barcelona kwa muda mrefu kabla ya kuhamia Paris Saint-Germain (PSG) mnamo 2021. Mwaka 2023, alijiunga na klabu ya Inter Miami nchini Marekani. Messi ameshinda tuzo nyingi, ikiwemo Ballon d'Or mara kadhaa, na alikuwa sehemu muhimu ya timu ya taifa ya Argentina iliyoshinda Kombe la Dunia 2022
Ufuatiliaji wa awali wa JamiiCheck umebaini video hii ya Messi akipiga gitaa iliwekwa Oktoba 7, 2024 kwenye ukurasa wa Instagram wa FutbolAlreves (tazama hapa).
UCHAMBUZI WA PICHA
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa Video hii imetengenezwa kwa Akili Mnemba kutokana na sababu zifuatazo
1. Vidole vya Lionel Messi havina umbo la kawaida, vinaonekana kama vimevimba.
2. Mijongeo na watu wanaopita nyuma ya Messi Wana Kasi kubwa isiyo ya kawaida.
Je, wewe umeona nini kingine?