Lionel Messi Hana Sifa za Uongozi kama za Cristiano Ronaldo

Nafikiri mkuu jibu linafanana, ana magoli mengi sababu ni proffesional wa kuzifunga timu ndogo, na nakupa sababu kwanini magoli ya makundi hayana faida zaidi ya Magoli ya hatua za mtoao, au kufunga Goli 3 mechi ambayo mmeshinda 7 Haina maana kuliko kufunga Goli 1 mechi mnayoshinda Goli 1.

1.Kwenye hatua za mtoano unakutana na Timu ngumu, Hakuna wakati Kama huu wa kusaidia timu yako, na hapa ndio wale Great players of all time utaona Wana shine, Kina Maradona Pelle, Zidane Etc Haingii akilini uniambie anayefunga Goli hatua ya makundi ni sawa na anayefunga robo/nusu/fainali, Iniesta mpaka leo tunamkumbuka kwa Goli lake, Gotze japo Hana career nzuri lakini atakumbukwa vizazi na Vizazi.

Mfano 2014 Messi kawafunga Bosnia, Iran na Nigeria, then alivyokutana na Uholanzi, Ubelgiji na Ujerumani unamtafuta kwa Tochi, mkuu unahisi kabisa uzito wa hizi mechi ni sawa? Kwamba anastaili same credit?

2. Hatua za mtoano Zina pressure, ukifungwa out, na hapa ndipo unapomtofautisha mchezaji mzuri na Legend, mechi Kama hizi zenye pressure ndio unaona Zidane anapiga Goli la ajabu, Inzaghi katokea kusipojulikana na kufunga.

Na ukitaka zaidi mkuu naweza kukuekea stats za Messi na timu zilizoingia fainali UEFA ama kuchukua Kombe hivi karibuni, aka elite Elite teams uone average goals na stats nyengine zilivyo ovyo.
 
Embu kamfatilie messi copa America zote alizocheza kaifungia Argentina magoli mangapi hatua ya nusu na robo fainal.
Then messi ni playmaker.
Hata kombe la dunia 2014 alifunga km mbadala tu wa striker kuzingua.
Ila yeye ndie mlishaji mipira kivp umpime kihivyo?
Halafu futa kauli yako kusema anazifunga team ndogo ilhali ana Historia ya kuitoa Madrid uefa nusu fainal.
Kazifunga sana man United,man city,juventus,chelsea,bayern Munich,Liverpool hzo we utaziitaje team ndogo
 
Ronaldo kushinda haki yake kutokana na yeye mchezaji ndan ya 18box tu akirudi nyuma kukimbia tu.
Tofauti na messi yeye ndiye coordinator pale katikati
 

Mkuu maelezo/sababu unazotoa ni dhaifu sana na yamejaa uongo na yanaashiria chuki tu dhidi ya Messi hakuna kingine.

Kwamba Messi ni professional wa kuzifunga timu ndogo tu uko serious kweli?

Amewahi kuwafunga hatrick brazilna pia Uruguay,Spain,Chile,Portugal,Ecuador amewahi kuzifunga akiwa na timu ya taifa ya argentina je hizi nazo ni timu ndogo?

Haya njoo upande wa club, yeye ndio top scorer wa inayosemekana kuwa ni biggest clash in today’s football at club level(El classico) sasa je Real madrid nayo ni timu ndogo?

Zaidi ya hapo pia yeye ndio anaongoza kuzifunga zile top six teams za EPL kwenye champs league, mpaka sasa kazifunga magoli 25. Arsenal kawafunga mara 8,man utd mara 4,liverpool mara 2,Chelesea mara 3,Spurs mara 2,man city mara 6. Na anashika nafasi ya nne kwa kuzifunga hizi timu baada ya rooney,Aguero na hary kane kumbuka hapo achezei epl kama hao wengine. Sasa je, hizi timu nazo ziko kwenye category yako ya timu ndogo?

Kingine pia amewahi kuwafunga juve,ac millan na bayern kwenye UCL je, hawa nao ni wadogo?

Halafu unashangaza sana unaponiambia kuwa eti magoli ya mtoano hayana faida, kwa mtu yeyote wa mpira hapa anakushangaa sana. Hivi timu isipopata matokeo mazuri kwenye hatua ya mtoano itaweza kuendelea hatua inayofuata? na matokeo mazuri unayapataje bila kufunga magoli? ...Taifa stars hii hapa imeshiriki Afcon imeshindwa kufunga magoli ya kutosha na imeruhusu magoli ya kutosha, sasa je imefika wapi kama magoli ya hatua ya makundi hayana umuhimu?

Messi kutowafunga ujerumani,ubeligiji na uholanzi haimnyimi credit ya kuwa alikuwa na overall good performance kwenye michuano. Na ndio maana fifa wakampa golden ball kama player of the tournament kama fifa nao wangekuwa wana perspectives kama zako basi asingechukua ile tuzo na badala yake wangempa mario gotze ambaye alifunga fainali.

Chamwisho nikukumbushe tu, messi kawafunga bayern munich goli 2 kwenye nusu fainali ya UCL,kawafunga real madrid goli 2(tena moja wapo ni goli bora la muda wote kwenye el classico) kwenye nusu fainali UCL,kawafunga liverpool goli 2 kwenye nusu fainali ya UCL,kawafunga marekani kwenye nusu fainali ya copa america na pia amewahi kutoa assist ya goli muhimu lililofungwa na iniesta kwenye nusu fainali ya UCL dhidi ya chelsea.

Leta hizo stats unazozisema.
 
Ronaldo kushinda haki yake kutokana na yeye mchezaji ndan ya 18box tu akirudi nyuma kukimbia tu.
Tofauti na messi yeye ndiye coordinator pale katikati
Unless umeanza kuangalia mpira juzi, ila miaka yote Ronaldo ni Winger au wing forward unaweza muita, Man U alikuwa pembeni na Kati Akicheza Rooney/Tevez/Berbatov, Madrid Akiwa pembeni Kati Chicha/Raul/Benzema/Higuain Etc Ronaldo ameanza kucheseshwa Kati uzeeni Tena baada ya mbio kukata.
 
ngoja namba ziongee.

Tuanze na average goals ya Messi, tutumie stats zako za 0.83 per match ulizoeka.

1. Tuanze na Juventus.
Messi amekutana na Juventus Mara 5 mechi mbili za makundi na tatu mtoano.
-makundi mechi 2 ana Goli 2
-Mtoano mechi 3 ana Goli 0

Hivyo mechi 5 na Juve ana Goli 2 Tena za makundi, Maisha yake yote hajawahi wafunga Juve mtoano.

wastani 0.4

2.Chelsea
Mechi 10 wamekutana na Messi ana magoli 3, Tena magoli yenyewe hajayafunga kipindi Chelsea wanajulikana Kama Elites, Akicheza mechi 8 na Chelsea ile Kali akiwa na Magoli 0

wastani 0.3

3. Bayern Munich
Mechi 5 Goli 4, hapa kidogo wastani wa magoli unalingana na wastani wa mechi zote.

wastani 0.8

4. Liverpool
Mechi 4 Goli 2

wastani 0.5

5.Real Madrid
Wamecheza mechi nyingi it's pointless even kuhesabu sababu Kuna Hadi vikombe vya mbuzi
Mechi 41 Goli 26

wastani 0.6

6. Atletico Madrid
Messi Mara Zote Akikutana na Atletico Uefa anashindwa kuwafunga, wamekutana Mara 4 na Goli 0 ila kwenye Ligi amewafunga tu kwenye Ligi Goli 24 mechi 26, Kama Madrid tusimuwekee wastani wa 0 tu assume Hata ligi ni Elite level. Mechi 38 Goli 29
wastani 0.76

Mkuu Angalia mwenyewe Hakuna Timu Hata moja Elite ambayo inafika fainali Mara kwa Mara ama kubeba Ndoo kwa miaka ya karibuni ambayo Messi ana wastani mzuri kushinda wastani wake wa Mechi zote, je statement yangu bado imebase kwenye chuki ama uhalisia?

For comparison ya haraka haraka Ronaldo mwenye 0.7
-bayern mechi 8 Goli 9 wastani 1.1
-Juve mechi 7 Goli 10 wastani 1.4
-Atletico mechi 8 Goli 7 wastani 0.87
-liverpool mechi 3 Goli 1 wastani 0.3
-Chelsea mechi 1 Goli 1 wastani 1

Mechi pekee Ambayo Ronaldo unaweza kusema anaflop Top level ni Against Barcelona ambayo Hajawafunga kwenye Champions league.
 

Bro as yet you haven’t brought up any meaningful explanations to defend your claims that Messi isn’t big tie performer, you are actually still waffling by keep recycling the same lame arguments.

Kwa mujibu wa hizo data ulizoweka hapo juu;

unamaanisha kuwa Messi zile goli mbili alizowafunga Juve hatua ya makundi hazina maana yoyote ile zingekuwa na maana kama angewafunga fainali sio? na hata ile assist aliyoitoa ya goli la Neymar kwenye mechi ya fainali haina maana yoyote kabisa sio?

unamaanisha kuwa alipowafunga chelsea hivi karibuni goli zake hazina maana yoyote sababu chelsea ilikuwa tayari imechoka si ndio? ila zingekuwa na maana kama angewafunga akina lampard? na pia hata assists mbili ambazo amewahi kutoa kipindi hiyo chelsea ikiwa ni elite kama unavyosema hazikuwa na maana yoyote ile? kwa hiyo kumbe timu kubwa akizifunga zimechoka ila asipofunga uwezo wake mdogo sio?... unachekesha sana.

Mbona umeruka kutiririka hoja zako hapo dhidi ya bayern munich, kulingana na mtazamo ulio nao mimi naona hata hapo ulitakiwa useme hizo goli 4 aliifunga bayern munich isiyokuwa na juppe heynckes kwa maana nyingine aliifunga bayern munich ambayo aikuwa elite kwa kipindi hicho(according to your logic).

Hapo dhidi ya real madrid unaposema eti ni pointless sababu wamecheza mechi nyingi ndio pointless yenyewe, kwa maana hata hapo nilitegemea uchambue mechi muhimu walizokutana hasa hatua ya mtoano ndio uzizingatie kama ulivyofanya kule juu dhidi ya juve na chelsea, ila badala yake ukaamua kuskip maana hiyo logic yako uliyoanza nayo kule mwanzo hapa ni irrelevant

Halafu kumbe mechi muhimu alizocheza dhidi ya Atletico madrid ni zile walizokutana kwenye Uefa champs league tu? ila hizi zingine huku kwenye vikombe vya ndani hazina umuhimu na hazipaswi kuzitilia maanani sio? interesting joke.

Halafu kwanini hapa kwenye hizi data zako zijawaona manchester united? au alipowafunga goli la kichwa baada ya kumzidi Fernand urefu man u haikuwa kwenye elite level? na pia vile alipomtetemesha Furguson pale wembley man u haikuwa elite? na pia vile vile ile ilikuwa ni mechi ya makundi?

Alipowafunga real madrid kwenye nusu fainali pale bernabeu kabla hajaenda kumtetemesha Babu wa watu, real madrid haikuwa kwenye elite level?

Halafu unaposema eti kuwa hakuna timu iliyofanya vizuri kwenye champs league hii miaka ya karibuni ambayo messi ana wastani mzuri wa kuifunga ana wastani mzuri wa kuifunga unamaanisha nini hasa? haya hii hapo liverpool ambayo ndio bingwa wa UCL ana wastani wa 0.5 je huo sio wastani mzuri?

Pia kumbe una kubali Ronaldo ni flop? tena flop wa game kubwa kama el classico? sasa kwanini awe flop kama kweli yeye mpambanaji kwenye hatua muhimu?

Bado hujanijibu swali langu, kama timu isipofanya vizuri kwenye hatua ya makundi itafikaje fikaje kwenye hatua ya mtoano? na hili ifanye vizuri kwenye hatua ya mtoano, itafanya fanyaje bila kufunga magoli?

Chief mpaka sasa bado hujatoa sababu/hoja za maana na zenye ushawishi kuonesha kuwa Messi hastahili kupewa sifa anazopewa, sana sana naona unatoa hojaa dhaifu sana zilizojaa hisia na ziko mbali na uhalisia wa kile unachokisema.
 

winger? unamuangaliaga Ronaldo anavyocheza lakini kwa umakini?

Tangu lini winger akawa anacheza huku most touches anazopata ni ndani ya box la wapinzani?

Tangu lini winger akazidiwa idadi ya crosses na mabeki? akina coentrao,cavajal,marcelo.

Tangu lini winger akawa anaongoza kwa idadi ya kupiga vichwa wakati yeye ndio anatakiwa awe mleta mipira ya vichwa?

Ronaldo ameacha kucheza kama winger asilia tangu alipoondoka man u. Huku uzeeni ndio kabisa amekuwa filipo inzanghi kabisaa ni mtu wa tap-ins tu basi.
 
Huwezi tumia mechi moja ku argue data zote nimetiririka data kibao mechi kibao, mtu amecheza mechi 10 against opponent Fulani wewe utumie data moja kuvalidate, toa data zako hapa Kama hauna kwaheri, not interested ku argue maneno maneno.
 
Really mkuu? una argue Ronaldo Hakuwa Winger sababu ana Touch nyingi kwenye Box? Hivi Kuna Hata mashabiki wa Mpira anayejinasibu anajua Mpira na hajui Kama Ronaldo alikuwa Winga?

Hii ni career yake Ronaldo Hadi Sasa


Mechi 356 amecheza Kama Winga wa kushoto, 127 Kama striker wa Kati, mechi 113 Kama Winga wa kulia,

Nipe na wewe source ya kuaminika kwamba Ronaldo sio Winga yangu hii hapa nilipitia hio screenshot.


Na hizo stats za cross unazosema nazo nazileta hapa kwa hao wachezaji uliowataja kwenye upande wa cross. Siku hizi Kuna internet kudanganyana kumepitwa na wakati.

Nakupa angalau stats za miaka kadhaa Ronaldo Toka anakuja Madrid.

Ronaldo average Crosses
2010- 0.6
2011- 0.3
2012- 0.6
2013- 0.3
2014- 0.3
2015- 0.6
Source

Coentrao average Crosses
2010-hajakuja madrid
2011-0.2
2012-0.4
2013-0.3
2014-0.2
2015-0.7
Source

Marcelo Average crosses
2010- 0.4
2011- 0.4
2012- 0.6
2013- 0.9
2014- 1.1
2015- 1.4
Source

Hizo Ndio stats za cross Baina ya Hao watatu.

Msimu pekee ambao Coentrao amempita Ronaldo kwa cross ni wa 2015 Tena Coentrao Akicheza mechi 2 tu ndio maana average ni kubwa hivyo Overall Coentrao Madrid hajawahi kuwa mpiga cross nyingi kushinda Ronaldo

Na Marcelo katika Hio misimu 6 Kuna msimu kapitwa na Ronaldo na Kuna msimu wamelingana ma misimu 4 Marcelo ana Cross zaidi.

Sasa Niambie kwa stats hizo Ronaldo Hakuwa Winga Hakuwa akipiga cross?

Naomba na wewe vyanzo vya kueleweka utoe ushahidi wa maneno yako kuwa Ronaldo sio mpiga cross. Na sio maneno tupu unayoongea muda wote.
 

Kabla hatujaenda mbali tukianza na hizi hizi stats zako, hapo kwenye blue hauoni kwamba tayari huu ni udhibitisho tosha kuwa huyo Ronaldo ni winga ndio lakini huwanjani achezi kama winga kwa kitendo cha yeye kuzidiwa crosses na Marcelo tena kwa misimu 4?

Marcelo ambaye ni beki na jukumu lake kubwa ni kulinda anamzidi mipira ya cross mtu ambaye jukumu lake la kwanza ni kupiga cross ukiachilia mbali kufunga, sasa hapo tuamini Ronaldo anacheza kama winga asilia uwanjani?

Pia sijamaanisha kuwa Ronaldo hapigi crosses bali hoja yangu ni kuwa achezi kama winga asilia na badala yake anacheza zaidi kama mshambuliaji wa kati na ndio maana mara nyingi mpira ukiwa kwenye half ya wapinzani, yeye utamkuta tayari yuko ndani ya box anadubiri kufanya tap in. kwa uchezaji wake sio winga kabisa maana ni tofauti na tunavyowaona akina Dimaria au Ribbery wakicheza.
 
Huwezi tumia mechi moja ku argue data zote nimetiririka data kibao mechi kibao, mtu amecheza mechi 10 against opponent Fulani wewe utumie data moja kuvalidate, toa data zako hapa Kama hauna kwaheri, not interested ku argue maneno maneno.

Sasa mbona katika maelezo yako yooote tangu mwanzo wewe unatumia vimechi vichache vichache ambavyo unaona vina fit kwenye logic yako?

Tangu mwanzo tukiongelea timu za taifa alizokutana nazo messi unazitaja ujeruma,uholanzi na ubeligiji hili tu upate validation ya kile unachokiamini, sasa huoni kwamba kama ni makosa ya ufinyu wa data umeanza kuyafanya wewe?

Sijaona mahali ulipotaja manchester united mpaka huu mjadala umefika hapa na kwenye huu mjadala manchester united iko relevant sana tu, ila hujataka kuisusha hata kidogo maana inge invalidate madai yako tangu awali
 
Kila position unayoiona ipo uwanjani Kuna Aina zaidi ya 10 ya wachezaji usiforce Mchezaji unayemjua wewe Basi wachezaji wote wawe hivyo hivyo.

Ronaldo ni Winga mshambuliaji kingereza Wing forward Toka yupo Man United Mpaka anakuja Madrid, Ameanza kucheza Kama Mshambuliaji wa Kati mwishoni kwenye career yake. Nimekuekea ushahidi wa website maarufu ya Mpira kwamba amecheza mechi zaidi ya 300 Kama Winga wa kushoto ila wewe maneno matupu unataka upinge kwamba yeye ni striker.

Kwaheri, comment yangu ya mwisho hii.
 
Leo Mess ni God Of Football ..uyo CR7 ni King Of Football.

Ndo tofauti ilipo apo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…