ngoja namba ziongee.
Tuanze na average goals ya Messi, tutumie stats zako za 0.83 per match ulizoeka.
1. Tuanze na Juventus.
Messi amekutana na Juventus Mara 5 mechi mbili za makundi na tatu mtoano.
-makundi mechi 2 ana Goli 2
-Mtoano mechi 3 ana Goli 0
Hivyo mechi 5 na Juve ana Goli 2 Tena za makundi, Maisha yake yote hajawahi wafunga Juve mtoano.
wastani 0.4
2.Chelsea
Mechi 10 wamekutana na Messi ana magoli 3, Tena magoli yenyewe hajayafunga kipindi Chelsea wanajulikana Kama Elites, Akicheza mechi 8 na Chelsea ile Kali akiwa na Magoli 0
wastani 0.3
3. Bayern Munich
Mechi 5 Goli 4, hapa kidogo wastani wa magoli unalingana na wastani wa mechi zote.
wastani 0.8
4. Liverpool
Mechi 4 Goli 2
wastani 0.5
5.Real Madrid
Wamecheza mechi nyingi it's pointless even kuhesabu sababu Kuna Hadi vikombe vya mbuzi
Mechi 41 Goli 26
wastani 0.6
6. Atletico Madrid
Messi Mara Zote Akikutana na Atletico Uefa anashindwa kuwafunga, wamekutana Mara 4 na Goli 0 ila kwenye Ligi amewafunga tu kwenye Ligi Goli 24 mechi 26, Kama Madrid tusimuwekee wastani wa 0 tu assume Hata ligi ni Elite level. Mechi 38 Goli 29
wastani 0.76
Mkuu Angalia mwenyewe Hakuna Timu Hata moja Elite ambayo inafika fainali Mara kwa Mara ama kubeba Ndoo kwa miaka ya karibuni ambayo Messi ana wastani mzuri kushinda wastani wake wa Mechi zote, je statement yangu bado imebase kwenye chuki ama uhalisia?
For comparison ya haraka haraka Ronaldo mwenye 0.7
-bayern mechi 8 Goli 9 wastani 1.1
-Juve mechi 7 Goli 10 wastani 1.4
-Atletico mechi 8 Goli 7 wastani 0.87
-liverpool mechi 3 Goli 1 wastani 0.3
-Chelsea mechi 1 Goli 1 wastani 1
Mechi pekee Ambayo Ronaldo unaweza kusema anaflop Top level ni Against Barcelona ambayo Hajawafunga kwenye Champions league.
Bro as yet you haven’t brought up any meaningful explanations to defend your claims that Messi isn’t big tie performer, you are actually still waffling by keep recycling the same lame arguments.
Kwa mujibu wa hizo data ulizoweka hapo juu;
unamaanisha kuwa Messi zile goli mbili alizowafunga Juve hatua ya makundi hazina maana yoyote ile zingekuwa na maana kama angewafunga fainali sio? na hata ile assist aliyoitoa ya goli la Neymar kwenye mechi ya fainali haina maana yoyote kabisa sio?
unamaanisha kuwa alipowafunga chelsea hivi karibuni goli zake hazina maana yoyote sababu chelsea ilikuwa tayari imechoka si ndio? ila zingekuwa na maana kama angewafunga akina lampard? na pia hata assists mbili ambazo amewahi kutoa kipindi hiyo chelsea ikiwa ni elite kama unavyosema hazikuwa na maana yoyote ile? kwa hiyo kumbe timu kubwa akizifunga zimechoka ila asipofunga uwezo wake mdogo sio?... unachekesha sana.
Mbona umeruka kutiririka hoja zako hapo dhidi ya bayern munich, kulingana na mtazamo ulio nao mimi naona hata hapo ulitakiwa useme hizo goli 4 aliifunga bayern munich isiyokuwa na juppe heynckes kwa maana nyingine aliifunga bayern munich ambayo aikuwa elite kwa kipindi hicho(according to your logic).
Hapo dhidi ya real madrid unaposema eti ni pointless sababu wamecheza mechi nyingi ndio pointless yenyewe, kwa maana hata hapo nilitegemea uchambue mechi muhimu walizokutana hasa hatua ya mtoano ndio uzizingatie kama ulivyofanya kule juu dhidi ya juve na chelsea, ila badala yake ukaamua kuskip maana hiyo logic yako uliyoanza nayo kule mwanzo hapa ni irrelevant
Halafu kumbe mechi muhimu alizocheza dhidi ya Atletico madrid ni zile walizokutana kwenye Uefa champs league tu? ila hizi zingine huku kwenye vikombe vya ndani hazina umuhimu na hazipaswi kuzitilia maanani sio? interesting joke.
Halafu kwanini hapa kwenye hizi data zako zijawaona manchester united? au alipowafunga goli la kichwa baada ya kumzidi Fernand urefu man u haikuwa kwenye elite level? na pia vile alipomtetemesha Furguson pale wembley man u haikuwa elite? na pia vile vile ile ilikuwa ni mechi ya makundi?
Alipowafunga real madrid kwenye nusu fainali pale bernabeu kabla hajaenda kumtetemesha Babu wa watu, real madrid haikuwa kwenye elite level?
Halafu unaposema eti kuwa hakuna timu iliyofanya vizuri kwenye champs league hii miaka ya karibuni ambayo messi ana wastani mzuri wa kuifunga ana wastani mzuri wa kuifunga unamaanisha nini hasa? haya hii hapo liverpool ambayo ndio bingwa wa UCL ana wastani wa 0.5 je huo sio wastani mzuri?
Pia kumbe una kubali Ronaldo ni flop? tena flop wa game kubwa kama el classico? sasa kwanini awe flop kama kweli yeye mpambanaji kwenye hatua muhimu?
Bado hujanijibu swali langu, kama timu isipofanya vizuri kwenye hatua ya makundi itafikaje fikaje kwenye hatua ya mtoano? na hili ifanye vizuri kwenye hatua ya mtoano, itafanya fanyaje bila kufunga magoli?
Chief mpaka sasa bado hujatoa sababu/hoja za maana na zenye ushawishi kuonesha kuwa Messi hastahili kupewa sifa anazopewa, sana sana naona unatoa hojaa dhaifu sana zilizojaa hisia na ziko mbali na uhalisia wa kile unachokisema.