Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
Usiku mmoja wa 1987 kitongoji cha Rosario Centro nchini Argentina alizaliwa Lionel Andres Messi Cucittini 'La Purga' binadamu mmoja mlaini na mfupi aliyekuja duniani kutueleza mana ya soka.
.
Wala hatupaswi kumuasi muumba wetu, wala hatupaswi kukufuru, hizi sio zama za Mitume na Manabii hivyo hatupaswi kumuita Nabii wa Mpira, ila wenye hamu sana ni vyema tukamwita kiumbe cha ajabu (Alien) kutoka nje ya dunia yetu.
.
Mawazo na fikra kubwa za mashabiki na wahafidhina wa FC Barcelona 'Blaugrana' ni usiku ule wa majonzi March 24, 2016 siku hiyo gwiji wa soka la Uholanzi, Johanny Cruyff ambae ni muasisi wa La Masia ameaga dunia, walilia mno hawakuamini macho na masikio yao.
.
Wakati nipo Ghetto nimetulia kushuhudia pambano la Barca na Espanyol la 2005 Messi anaingia sub akiwa na number 19 mgongoni, hisia na fikra zangu zilienda mbali mno, kweli siku zinaenda mbio.
.
Nilijisemea tu, huyu ni Lionel Messi kipenzi chao, anaecheza mbele yao kumalizia burudani yao, simwoni Messi miaka minne mbele pale Nou Camp, muda wake unaishia.
.
Aliwahi kuaga kwa majonzi Xavi Hernandez, aliaga Don Andres Iniesta, ila vipi huyu binadamu siku anawapa mkono wa kwaheri, vipi ile siku Messi anavuta waya kwa Rais wa Barca kumpa taarifa.
.
Nawaza ile safari yake ya dakika 20 kutoka mitaa ya Castelldefels ile Mikocheni ya Jiji la Barcelona mpaka Nou Camp kuwaaga, bado nawaza afikapo mitaa ya Hesperia ilivyo na msongamano na watu wakitaka kujua hatma yake.
.
Nawaza hiyo siku Miguel Ruiz (Mpiga Picha wa Barcelona) akiweka memory kwenye Canon yake, akijua ni shot yake ya mwisho kwa Messi akiwa Barca, machozi yatamtoka ila hana namna.
.
Namuwaza sana Joaquim Maria Ortiga wa Radio Catalunya, alikuwa mtu wake wa karibu mno, atazimiss zile interview zake na ukaribu wao, Messi anasepa zake, wakati na saa umefika kuvua kitambaa cha Unahodha.
.
Juu kabisa wapo watoto wake na Mke wake kipenzi Antonella Rocuzzo, mwanae mtukutu Matheo atageuka na kumtazama Mama yake, "Mbona hachezi yupo tu mle uwanjani Baba?"
.
Futa tu machozi usilie, piga moyo konde zamu yake imeisha atakuja mwingine, hii ni Barcelona hii ni zaidi ya klabu 'Mes Que un club'.