'Lionel Messi Kurejea Nyumbani'

'Lionel Messi Kurejea Nyumbani'

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957
Wadau
Zimekuwepo tetesi za muda kuwa 'Lionel Messi' anampango wa kurejea nyumbani. Taarifa hizi zimekanushwa na yeye mwenyewe aliyesema kuwa hana mpango wa kuhama kutoka katika klabu yake ya sasa ambayo ameitumikia kwa muda Mfupi Sana.
Hata hivyo taarifa kutoka vyanzo vya uhakika zinasema 'superstar 'huyo amedhamiria kuondoka na yupo katika hatua za mwisho kabisa kurejea ''Buenos Aires''.Kuondoka kwake kumecheleweshwa baada ya ''Wakala Mkuu' wa mchezaji huyo kuvujisha siri hiyo bila kudhamiria kutokana na furaha kubwa aliyokuwa nayo baada ya kupata ridhaa yake.'Mshambuliaji huyo mwenye haiba ya upole na ukimya ana sifa ya weledi mkubwa wa kupanga na kufanikisha mashambulizi dhidi ya Adui.Mchezaji huyo mara atakaporejea nyumbani atakabidhiwa kazi ya kuwa mshauri wa Kamati ya Ufundi.
Vyanzo makini makini vinasema ni suala la muda hivyo wapenzi wa ''soka'' wawe na subira.
Karibuni
Latest:
Taarifa Za Hivi Punde Zinasema Mchezaji Huyo Tayari Ameomba Asijumuishwe Kwenye Kinyang'anyiro Cha Tuzo Ya Uchezaji Bora. Ameomba Nafasi hiyo Apewe "C.R.7"
 
duh kama ni hivyo 2020 kutakua na uchaguzi wa kura za ndio/hapana
 
Hebu katizameni Barca anavyolambishwa udongo na Valencia mida hii
 
tena nimesikia "messi" huyo anataka kurudi "argentina" alikozaliwa. eti anahisi yupo uhamishoni na hapendi hali hiyo. dah, ila bora ahame atuachie "baselona yetu" dah! lakini tutafanyaje na "neymar" tumemuuza "psg" na juzi tu bosi wake amempa u kapteni? inauma sana. ila ngoja tuanze kujenga upya timu yetu. ndo muda wetu na sisi wa kuwa hata wachezaji wa akiba! ngoja nianze mazoezi mdogomdogo. pi..z..! da! ntaweza kujaza uwanja kama "mesi"?
 
Back
Top Bottom