Lionel Messi ni mchezaji wa ajabu

Joined
Oct 26, 2021
Posts
99
Reaction score
294

Baadhi ya makocha na wachezaji wa zamani wamemzungumzia Messi Kwa aina tofauti:
๐Œ๐ข๐œ๐ก๐š๐ž๐ฅ ๐Ž๐ฐ๐ž๐ง: "Sifikirii mtu yeyote anaweza kucheza mchezo wa soka kama vile Messi."
๐…๐ซ๐š๐ง๐ค ๐‘๐ข๐›๐ž๐ซ๐ฒ: "Messi ni darasa. Kuna yeye, halafu kuna wengine."
๐’๐š๐ฆ๐ฎ๐ž๐ฅ ๐„๐ญ๐จโ€™๐จ: "Lionel Messi ni Mungu, kama mtu na hata zaidi kama mchezaji."
๐—๐š๐ฏ๐ข ๐‡๐ž๐ซ๐ง๐š๐ง๐๐ž๐ณ : "Ni wazi kuwa Messi yuko katika kiwango cha juu kuliko wengine wote. Wale wasioona hayo ni vipofu."
๐‚๐š๐ซ๐ฅ๐ž๐ฌ ๐๐ฎ๐ฒ๐จ๐ฅ: "Lionel Messi yuko juu kuliko kitu kingine chochote ambacho nimewahi kuona. Yeye ni mgeni."
๐ƒ๐ข๐ž๐ ๐จ ๐Œ๐š๐ซ๐š๐๐จ๐ง๐š: "Nimeona mchezaji ambaye atarithi nafasi yangu katika soka la Argentina ni Lionel Messi. Messi ni gwiji."
๐‰๐จ๐ฌ๐ž ๐Œ๐จ๐ฎ๐ซ๐ข๐ง๐ก๐จ: "Messi anapokuwa na mpira, mmoja mmoja, umekufa."
๐‹๐ฎ๐ข๐ฌ ๐„๐ง๐ซ๐ข๐ช๐ฎ๐ž: "Bila shaka, Lionel Messi ndiye bora zaidi duniani kwangu."
๐๐ž๐ฉ ๐†๐ฎ๐š๐ซ๐๐ข๐จ๐ฅ๐š: "Usiandike kumhusu, usijaribu kumwelezea. Mtazame tu!"
๐’๐ž๐ซ๐ ๐ข๐จ ๐€๐ ๐ฎ๐ž๐ซ๐จ: "Nimekuwa Ulaya kwa miaka 15 na sijaona mtu kama Messi, hakuna mtu anayekaribia!"
๐Œ๐š๐ซ๐œ๐จ ๐•๐š๐ง ๐๐š๐ฌ๐ญ๐ž๐ง: "Cristiano ni mchezaji mzuri, lakini wale wanaosema yeye ni bora kuliko Messi hawajui lolote kuhusu soka."
๐†๐ข๐จ๐ซ๐ ๐ข๐จ ๐‚๐ก๐ข๐ž๐ฅ๐ฅ๐ข๐ง๐ข: "Ili kumzuia Cristiano Ronaldo, inabidi umzuie asipate mpira kwenye kisanduku, Ili kumzuia Lionel Messi, unatakiwa kuomba, maana hazuiliki."
 
Kipaji anacho ila Ronaldo the goal scorer ndo funga kazi wangu
 
Jamaa napenda zile moves zake tu ule mpira kama umenata kweny mguu na anavyodribble...anavile vitobo vyake akama alichmpiga James milner guardiola akashangaa ...jamaa ni hatar sana chenga zake yaani anapita fasta katoboa
 
Messi ni bora wa muda wote hakuna mchezaji anamkaribia kwa zamani na sasa

Na kwa kizazi hiki cha dawa na chips ni vigumu kupata talent zaidi yake
 
Tofautisha kati ya hivi vitu viwili kipaji na juhudi Messi ana kipaji asilia au tuseme Cha kuzaliwa Ronaldo ana juhudi na mazoezi pia yanachangia anajituma sawa sawa useme ..

Alikiba vs diamond alikiba ni kipaji diamond ni juhudi Na ubunifu.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Kipaji anacho ila Ronaldo the goal scorer ndo funga kazi wangu
Ronaldo ni magoli tu (ambayo anazidiwa na messi ukiangalia idadi ya mechi walizocheza)
Messi ni kila kitu
 
Nashangaaga watu wakiulizwa top 3 ya wachezaji bora of all time utasikia majina ma3 yanayozungumziwa... Pele, Messi,na Maradona, Na kwenye jayo majina Messi wanampa namba moja.

Halafu tena baadae haohao watu wanakaa chini kudiscuss nani bora kati ya messi na Ronaldo?? WTF๐Ÿค”
 
Juhudi mtu yeyote anaweza kufanya akafikia hiko kiwango, hata haaland akijitahidi anaweza kufika level za ronaldo.
ila Messi ni impossible.
Wewe fikiria mnasema Messi sio goal machine lakini ndio anashika rekodi ya kufunga magoli mengi kwa mwaka 1 (90)
 
Yule was kwetu amebaki Singano jina alilopewaga limemzidi kimo
 
Point Yako ni ipi mkuu

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Hivi huu ujinga wa kusema Ronaldo ana juhudi sio kipaji nani aliuanzisha?

Hebu jaribu na wewe kufanya juhudi tuone kama utakuwa kama Ronaldo.

Ronaldo ana kipaji cha mpira hilo halina shaka. Sema Messi ana kipaji zaidi ya Ronaldo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ