Guantanamo Sobibor
JF-Expert Member
- Aug 20, 2017
- 897
- 1,133
Ni sawa Ronaldo kachukua Euro sikatai lakini ninachotaka kusema ni kwamba Messi anakosa bahati katika fainali hizo zote pamoja na uzembe wa baadhi ya wachezaji wenzie kama vile Higuain alipokosa one against one mara mbili dhidi ya Neuer fainali ya 2014.Katika timu hata uwe unaujua mpira vipi huwezi kuibeba timu peke yako bila msaaada wa wachezaji wenzio kumi.Kama mfuatiliaji mzuri wa timu ya taifa ya Argentina Messi anajitolea sana lakini kuna baadhi ya wachezaji wanamuangusha.Messi siyo malaika kusema atacheza vizuri makundi,round of 16,robo fainali,nusu fainali hadi fainali.At a certain point itabidi mtu mwengine afanye kitu endapo yeye ameshindwa kufanya kitu hata Ronaldo wakati anachukua Euro aliisaidia Ureno hadi nusu fainali kufika fainali kapata majeraha mapema kashindwa kuendelea na mchezo lakini wenzie hawakumuangusha tofauti na Argentina Messi anafanya kazi kubwa sana wakati wenzie wanajificha katika kivuli chake.Ronaldo Kaichukulisha Ureno (Trophy) EURO moja kwa Fainali moja....
FAINALI 4 BILA YA KOMBE KAZI BURE....
FAINALI MOJA TU YENYE KOMBE NI BORA KULIKO 100000 ZISIZO NA KOMBE....
Kumbuka Messi Kaifikisha Aregentina Fainali 4 za Coper America & World Cup na Kusumbuliwa Na Watoto Wa Dogo Kina Chile na Uruguay, Tena Kibaya Zaidi Alisumbuliwa na Wale watoto Wa Brazil Waliotandikwa Goli 7 na Ujerumani...
Hivi Mkuu Ujerumani Kamroga Wapi Argentina Hata ikafika Pahala Kuwa Popote Anapomkuta Anamdonoa?
Mwaka 1990 Fainali World Cup Ujerumani vs Argentina ... Ujerumani Kaibuka Kidedea.
Mwaka 2014 Finali World Cup Ujerumani vs Argentina... Ujerumani Kaibuka Kidedea...
2006 World Cup Robo/Au 16 bora Ujerumani na Argentina... Ujrumani Kaibuka Kidedea..
Yaani Argentina na Messi Wake Kwa Ujerumani ni Nyanya tu..
Fainali Mbili Zote Anafungwa na Ujerumani anashindwa Kujikomboa?
MY TAKE:
RONALDO na MESSI wote Watastaafu SOKA bila Ya Kubeba World Cup Kwani 2018 ni Vita Vya Wababe WANNE tu...
1) UJERUMANI
2) BRAZIL
3) UFARANSA
4) UENGEREZA
Waliobakia Kina Spain, Italy na Argentina ni Wasindikizaji tu.
Katika hiyo list yako muondoe Uingereza hamna timu humo ni mkusanyiko wa wachezaji wenye majina makubwa tu na wanaopambwa na sky sports na vyombo vyao vyengine vya habari,hao zao mechi za kirafiki tu halafu never write off the likes of Spain na Belgium wana vikosi na timu nzuri.