Akilihuru
JF-Expert Member
- May 20, 2022
- 1,512
- 2,980
Habari ya mchana huu wakuu, leo nimekuja na historia ya huyu mwamba na mtawala wa aina mbali mbali za miziki laini, yan ile inayogusa mioyo ya mamilioni ya wapenzi wa miziki hapa duniani.
Aina hizo za miziki ni funk, soul, rhythm, blues and country.
Anaitwa Lionel Brockman Richie Jr (born June 20, 1949) huko Alabama, USA.
Lionel Richie ni miongoni mwa wasanii walioanza kuimba wakiwa na umri mdogo kabisa, ambapo yey alianza kujishughulisha na mziki akiwa na umri wa miaka 12 tu, na ni miongoni mwa waimbaji wenye kipaji cha uimbaji na utungaji.
Lionel Richie ana sauti ya pekee ambayo inaweza kumgusa mtu yoyote moyoni hata kama kile anachoimba haukielewi.
Ni mmoja kati ya wasanii wachache waliofanikiwa kuteka akili, na kugusa mioyo ya mamilioni ya watu mbali mbali duniani kutokana na ubora wa nyimbo zake, umaridadi wake, sauti yake na pia aina ya uimbaji wake.
Mnamo miaka ya 1985s Lionel Richie ndio alimshauri Michael Jackson kutunga ule wimbo wa "We Are the World" ili fedha zitakazopatikana katika wimbo ule ziweze kusaidia watoto wenye matatizo mbali mbali duniani kama vile yatima, wagonjwa na wale wenye uhitaji wa msaada.
Baadhi ya vibao vyake kati ya vyote vilivyo bora ni 👇
1) Endless love ft Diana Ross.
2) Ballerina girl.
3) Stuck on you.
4) Say you, Say me.
5) All Night Long.
6) We Are the World & Michael Jackson na wengine.
Kwa wale wazee wa miziki laini, nafikiri mnamjua vizuri mwamba huyu kwa sauti na uimbaji wake.
Kazi yake kubwa ni muimbaji, muandikaji wa nyimbo mbali mbali na ni mtungaji mahiri sana.
Karibuni wakuu tujadili na mengine mnayoyajua kumhusu mwamba huyu wa soft songs.