Lionel Ritchie anaendelea vizuri baada ya kukimbizwa na kulazwa hospitalini

Lionel Ritchie anaendelea vizuri baada ya kukimbizwa na kulazwa hospitalini

loose Nut

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
2,887
Reaction score
6,657
Mwanamziki mkongwe maarufu mmarekani ambye nyimbo zake hazichuji Lionel Richie 78, anaendelea vizuri baada ya kukimbizwa hospitalini.

Alikuwa akitumbuiza stejini jijini St. Paul Minnesota nakushikwa na kizunguzungu na kupelekea wauguzi kumuwahisha hospitalini.

Gwiji huyo wa miondoko ya Soul and R&B alitamba na Nyimbo za Stuck on you na Hello ambazo tumezaliwa tumezikuta hadi sasa hivi ni watu wazima bado hazijachuja.

Pia Lionel pamoja na marehemu Michael Jackson (Mitchell Jacques) kifaransa walitunga wimbo maarufu we are the world.

Kula chuma hicho hapo chini Hello!



Senior JF Producer and entertainment master

adriz de mbusii
 
Mwamba sana huyu na umri wake umeenda sasa, miaka 77 siyo haba.
Kibao chake cha All night long kilikubalika sana miaka hiyo hasa kutokana kipande cha maneno ya kiswahili yaliyowekwa kwenye wimbo huo. "Jambo nipe senti moja"
 
Mwamba sana huyu na umri wake umeenda sasa, miaka 77 siyo aba.
Kibao chake cha All night long kilikubalika sana miaka hiyo hasa kutokana kipande cha maneno ya kiswahili yaliyowekwa kwenye wimbo huo. "Jambo nipe senti moja"
Really I didn't know this. Asante kwa kutufahamisha mtu wangu.
 
All night long.

All night.

All night

All niiiiiiiight.

Mojawapo ya kibao pendwa cha nguli huyu.
 
Nje ya mada.

Mtoa mada twende tukahangaike Sasa kwenye uzi wa WC maana muda ushakaribia
 
Wataalamu wa Afya waseme...umri zaidi ya miaka 75 inafaa mtu ku-perform kujwaani kama wasanii wengine?
 
Vijana wa zamani tumemfaidi sana huyu mwamba. Enzi hizo uko geto halafu umeweka nyimbo za blues.. macho yote yameganda mlangoni kumsubiria mgeni agonge.
 
Back
Top Bottom