Lipi chaguo sahii? Tafadhali nishauri

Lipi chaguo sahii? Tafadhali nishauri

mbukoi

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2012
Posts
455
Reaction score
443
Heshima kwenu wakuu? Ninawashukuru sana wazoefu wa magari kwa elimu mnayotoa humu jukwaani inayosaidia kutoa tongongo kwa mimi ambaye uelewa wangu kwenye mambo haya siyo mkubwa.
nirudi kwenye mada.
Nimejikusanya na kutunza kiasi cha 4ml kwa ajili ya usafiri utakaoniwezesha kutoka nyumbani kwangu kwenda kazini kila siku umbali wa km 16 kwenda na kurudi na pia mara moja kwa wiki kufuatilia shughuli zangu zingine umbali wa kati ya 50 km hadi 120 km kwenda na kurudi (ni route mbili tofauti).
Kwa kuzingatia ulaji wa mafuta, fueli economy, maintanance cost na comfortability naomba mnishauri kati ya machaguo haya ambayo tayari ninayo: Corrola E 111 corrolla 110 na Carina ti.
Natanguliza shukrani wadau.
 
Kila la kheri mkuu, ukinikuta barabarani usiache kunipa lift
 
Hizo gari zote tofauti ni ndogo saana. Japo sijaelewa kwenye Corolla sijaelewa ni AE110 au AE111. Kama ni 111, haina mwonekano mzuri. Ukipata AE110 manual go for it. Ukikosa, chukua Ti.
 
Kwa dau hilo utapata Corolla nzuri,lakini carina itakubidi uwe mpole au uongeze dau kidogo au unaweza kupata ambayo haiko katika hali nzuri, sasa basi kwa kwa kuwa hizo gari zote hazina utofauti mkubwa mm nakushauri bila kujali muonekano nenda jitwalie Corolla.
 
Hizo gari zote tofauti ni ndogo saana. Japo sijaelewa kwenye Corolla sijaelewa ni AE110 au AE111. Kama ni 111, haina mwonekano mzuri. Ukipata AE110 manual go for it. Ukikosa, chukua Ti.
Ahsante sana kwa ushauri mkuu. AE 110 Automatic ina shida gani mkuu?
 
Kwa dau hilo utapata Corolla nzuri,lakini carina itakubidi uwe mpole au uongeze dau kidogo au unaweza kupata ambayo haiko katika hali nzuri, sasa basi kwa kwa kuwa hizo gari zote hazina utofauti mkubwa mm nakushauri bila kujali muonekano nenda jitwalie Corolla.
[/QUO
Ahsante sana mkuu. Sihitaji yenye hali mbaya mkuu kwani ni gari yangu ya kwanza ikiniambia itakuwa shida. Carina yenye hali nzuri ntahitaji kuongeza ngapi? Kwanini bei ya Carina iko juu? Ina nini cha ziada ukilinganisha na corrola?
 
Ahsante sana kwa ushauri mkuu. AE 110 Automatic ina shida gani mkuu?
Vile hazipo saana mtaani sasa hivi, utapata ya zamani, na nyingi zimetumika kama taxi. So manual mara nyingi inavumilia shida zaidi. Ila kama iko kwenye hali nzuri, auto haina shida kabisa.
 
Vile hazipo saana mtaani sasa hivi, utapata ya zamani, na nyingi zimetumika kama taxi. So manual mara nyingi inavumilia shida zaidi. Ila kama iko kwenye hali nzuri, auto haina shida kabisa.
Ahsante sana mkuu
 
Back
Top Bottom