Wakuu wana bodi,
Ni muda mrefu sijapost thread hapa,ila leo wakati tukiendelea kuisubiria Sikukua ya kuzaliwa kwa bwana Yesu Kristo nimeona ni vyema kuanza na thread hii.
Binafsi nampongeza mhe. Rais kwa kuweza kuliongoza taifa letu kwa miaka Minne,tumepitia mambo mengi ,msikusuko mingi na mambo kadha wa kadha.
Ila leo yakiwa yamepita masaa 48 ningependa tukumbushane ni yapi mazuri aliyofanya na yapi tunaona ni wa kati muafaka kumshauri mhe. Rais ayafanyie kazi kw akipindi cha mwaka mmoja ujao.
naomba tujadili..
Btw the Line,I smell something fishy on ATCL.Stay tuned!
Mazuri ambayo yanatakiwa yaendelezwe:
1. Amesimamia ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma
2. Ametoa uhuru wa watu kutoa maoni yao hata yale ambayo yanampinga moja kwa moja. Mkapa alikuwa akiminya uhuru wa vyombo vya habari na alidiriki hata kuwakashfu Wakati wa mahojiano yake na Riz Khan wa CNN wakati huo.
3. Amewaruhusu wabunge wa CCM kuongea kwa uwazi zaidi bila ya vitisho - utakumbuka kuwa Rais mstaafu Mkapa aliwafunga midomo wabunge hawa wanaojiita wapiganaji wa ufisadi na walifyata mkia.
4. Ameruhusu baadhi ya mafisadi kufunguliwa kesi mahakamani - refer Mramba, Yona, Mgonja etc.
5. Alikuwa radhi Baraza lake la mawaziri na hasa waziri mkuu ajiuzuru baada ya kashfa ya Richmond
6. Ameipa meno zaidi ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali (CAG) ambayo imekuwa chanzo cha kugundulika kwa kashfa nyingi tunazozijua hivi leo.
7. Ameendeleza uhusiano mwema wa Tanzania na majirani zetu na aliweza kuwa kiungo muhimu wakati wa mgogoro wa Kenya tofauti na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pamoja aliamua kuegemea upande mmoja.
Mapungufu ambayo yanahitaji marekebisho
1. Vita dhidi ya ufisadi ambayo kwa sasa Serikali imekuwa legelege has katika kuchunguza na kuwafungulia mashitaka watuhumiwa. Serikali imekuwa ikilalamika zaidi ya kuchukua hatua.
2. Safari nyingi za nje na ndani ya nchi ambazo tija yake ni vigumu kuitathmini.
3. Kushindwa kukamilisha kwa wakati miradi mikubwa ya barabara ambayo aliirithi toka kwa mkapa ikiwepo barabara ya kati ya Manyoni na Singida na barabara ya kusini.
4. Kuendesha nchi kwa kauli mbiu ambazo hazina mipango kamili ya utekelezaji wala usimamizi - Kilimo Kwanza, Nguvu mpya ari mpya na kasi mpya ni baadhi ya kauli mbiu hizo.
5. Kuendeleza matumizi mabaya ya fedha za umma kwa ugawa fedha kiholela bila kuwa na utaratibu unaoeleweka wa kizisimamia na kujua impact yake kwenye jamii - refer Mabilioni ya Kikwete (Tshs 21 billion)
6. Kutoa matamshi ambayo yanatiashaka na umakini wa Serikali katika kusimamia sheria za nchi - mf. madai kuwa ana majina ya wala rushwa, majambazi na wakwepa kodi kuwa anawapa muda wajirekebishe.
7. Kutotekeleza ahadi za wakati na baada ya kampeni - mfano ni ile ya kurudisha nyumba za Serikali hasa zilizo katika maeneo yenye taasisi nyeti zilizoporwa na Mkapa, Magufuli na mafisadi wengine wa awamu ya tatu.
8. Kuendeleza sera potofu za awamu ya tatu za kukumbatia wageni - waliobatizwa kuwa wawekezaji - na kuwakandamizi wananchi wa hali ya chini. Refer wananchi wa Babati wanaohamishwa kwenye maeneo yao kupisha mwekezaji.
Naamini kuwa mapungufu haya yanarekebishika ikiwa Rais ataamua kwa dhati ku