Lipi neno sahihi kati "SAINI na SAHIHI?

Lipi neno sahihi kati "SAINI na SAHIHI?

Naomba kujua matumizi ya hayo maneno kuoneshe "signature" lipi ni rasimi?
Saini(Sign) ni kiingereza ambapo ni kifupi cha signature,Sahihi ni kiswahili

Watu huwa wanachanganya lugha bila kujijua ila hakuna neno Saini kwenye kamusi ya kiswahili sanifu bali kuna neno Sahihi.
 
Ni sahihi kutumia neno saini kumaanisha Signature
 
Saini ndiyo signature isipokuwa neno sahihi limeathiriwa na lahaja tofauti. Ila linatumika katika matumizi katika mikataba.
Kwa maana halisi ya kiingereza sahihi means something correct.
 
Sign - kiashiria cha utambulisho wa jambo, nomino nk, signature - uthibitisho wa utambulisho, kutambuliwa.
 
Yote sahihi ila matumizi ni tofauti

In eng
Saini means put a signature
Sahihi=signature
Na mm nina mawazo kama yako Saini (kitendo).Mtu atakwambia saini hapa (yaani weka sahihi,ule mwandiko wa kunyonanyonga...).Sign(saini)=Verb(Kitendo).Sahihi kwenye kiswahili linaweza kutumika kama Correct au Signature hapo ndipo tatizo lilipo!!
 
Yote maneno mawili ni kiswahili sawa tu yanatumika kama ifuatavyo.
Saini ni kitenzi na sahihi ni nomino ya hicho kitenzi.
Baba amesaini barua zote muhimu.
Kitenzi
Baba anasaini barua zetu sasa hivi
Kitenzi
Baba ana sahihi nzuri sana
Nonimo
Sahihi ya baba ni ngumu kuidurufu
Nomino
Sahihi=signature
Saini=sign

I was signing very important documents
I was putting my signature to Juma's documents
This document was signed by James
This is James signature.
 
Maneno mawili 'saini' na 'sahihi' Kimsingi yanatofautiana, saini kwa kisukuma huitwa signature(sign) na sahihi wasukuma wanaita something correct, right.
Kuna watu wanatumia maneno haya kimazoea tu.
 
Maneno mawili 'saini' na 'sahihi' Kimsingi yanatofautiana, saini kwa kisukuma huitwa signature(sign) na sahihi wasukuma wanaita something correct, right.
Kuna watu wanatumia maneno haya kimazoea tu.
Sio kweli, saini=sign na sahihi =signature ila neno sahihi lina maana mbili sahihi = correct
Ni sawa na neno shuka pia lina maana mbili shuka = drop na shuka = bedcover
 
saini ni neno la kingereza (sign), likimaanisha kutia sahihi.. sahihi ni kiswahili fasaha ambacho kinamaaniasha (signature)
 
Saini in kitenzi na sahihi ni nomino japo yanatumika bila kujua.
MF: Nilimambia asaini hapa. Yaani afanye kitendo cha kuqeka sahihi.
Au
Nilimwambia aweke sahihi yake hapa. Yaani sahihi ni nomino
 
MFANO...Weka SAHIHI yako hapa...... OKWI amesaini Simba....huwezi sema okwi amesahihi simba.....nadhani yote ni sawa ila kwenye kutumia ndy yanabadilika
 
Yote ni sawa ila kuna tofauti kwenye matumizi
saini hutumiwa kama verb/tendo mara nyingi
Bwana juma amesaini mkataba wa mika miwili

na sahihi hutumika kwa kiswahili fasaha na hutumiwa kama noun
hii ni sahihi ya bwana Juma

*** sahihi pia hutumika kuonesha mtu ypo sawia na asemacho***
Bwana Juma yupo sahihi kabisa.
 
Back
Top Bottom