Lipi neno sahihi "shusha" na "acha"

Lipi neno sahihi "shusha" na "acha"

Focas Kamali

Member
Joined
Jun 13, 2012
Posts
12
Reaction score
3
Mara nyingi ndani ya vyombo vya usafiri hasa daladala utasikia abiria anatamka shusha kituo fulani ama acha kituo fulani. Ni neno gani hasa linapasa kutumika?
 
Kusema kweli lugha sahihi ni 'shusha' au pengine 'teremsha'

Lakini kama ujuavyo makonda na wafanyakazi mahotelini wana lugha yao tunayoielewa lakini si rasmi. Konda akisema 'Mpe gari huyo' sote tunajua maana yake halikadhalika muuza hoteli anaposema 'nipe ng'ombe mmoja na cheche'
 
Kama unataka kujadili katika muktadha uliouwakilisha, neno sahihi ni "SHUKA" au "TEREMKA" na wala sio SHUSHA au ACHA.

Hivyo mtumiaji wa chombo cha usafiri mathalani anapaswa atamke ya kwamba:

Nahitaji kushuka mahali fulani au Nahitaji kuteremka mahali fulani.
 
Shusha ndio nene sahihi abiria atatamka shusha kituo fulani kwa kuwa kuna mtu atatermka pale konda ndiye atasema shuka dada au mama
 
neno linaloweza kutumika hapo hasa kwa wakati huo wa usafiri ni shusha kwani shusha linamaana ya kushushakitu toka sehemu moja na kwenda sehemu ingine hivyo neno shusha lafaaa zaidi kimtazamo wangu
Mara nyingi ndani ya vyombo vya usafiri hasa daladala utasikia abiria anatamka shusha kituo fulani ama acha kituo fulani. Ni neno gani hasa linapasa kutumika?
 
Kama unataka kujadili katika muktadha uliouwakilisha, neno sahihi ni "SHUKA" au "TEREMKA" na wala sio SHUSHA au ACHA.

Hivyo mtumiaji wa chombo cha usafiri mathalani anapaswa atamke ya kwamba:

Nahitaji kushuka mahali fulani au Nahitaji kuteremka mahali fulani.

Neno sahihi kwa abiria kulitumia katika kumtaarifu kondakta au dereva ni 'Shusha!Kimsingi hiyo ni 'Amri' kutoka kwa abiria:na amri hii inaweza kutolewa moja kwa moja na abiria bila kondakta au dereva kuuliza au baada ya kondakta au dereva kuuliza kuhusu kama kuna abiria yeyote anataka kushuka ktk kituo husika.

Na abiria akilitumia neno "Shusha" kunaweza kukawa na maana mbili:-
1.Huyo abiria aliyetamka shusha anataka kushuka ktk kituo hicho.
2.Huyo abiria aliyetamka shusha anayo taarifa kua kuna abiria mwinzie anataka kushuka katika kituo hicho;
Ila neno "Shusha" likitumika walau abiria mmoja ashuke ktk kituo husika:Na sio lazima kwa abiria aliyetamka neno "shusha" ashuke.

Neno 'Acha' sio neno fasaha la kumtaarifu kondakta au dereva kuhusu maamuzi ya abiria ya kutaka kushuka kwenye kituo fulani.
 
una akili kama zangu wewe

Back
Top Bottom