DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameshangazwa na ushindi wa asilimia 97 aliopatikana na mgombea wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025. Lipumba amesema kuwa ni ushindi mkubwa ambao haujawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, na kuibua maswali akibainisha kwamba kama kweli CCM inapendwa na wananchi pamoja na mgombea wake, kwa nini serikali inahofia maandamano, na kwa nini aapishwe kinyemela bila wapiga kura?.
Amesema" Matokeo yaliyotangazwa haya wakilishi uhalisia wa kura zilizopigwa, ni matokeo ya kupikwa yamevunja misingi ya haki, uwazi na uhalali wa kidemokrasia serikali imepoteza kabisa imani kwa wananchi ndani na nje ya nchi".
Ameyasema hayo Novemba 5, 2025, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam.