PostGE2025 Lipumba: Kama CCM na Samia wanapendwa na wananchi kwanini aliapishwa KINYEMELA?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameshangazwa na ushindi wa asilimia 97 aliopatikana na mgombea wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025. Lipumba amesema kuwa ni ushindi mkubwa ambao haujawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, na kuibua maswali akibainisha kwamba kama kweli CCM inapendwa na wananchi pamoja na mgombea wake, kwa nini serikali inahofia maandamano, na kwa nini aapishwe kinyemela bila wapiga kura?.

Amesema" Matokeo yaliyotangazwa haya wakilishi uhalisia wa kura zilizopigwa, ni matokeo ya kupikwa yamevunja misingi ya haki, uwazi na uhalali wa kidemokrasia serikali imepoteza kabisa imani kwa wananchi ndani na nje ya nchi".

Ameyasema hayo Novemba 5, 2025, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam.
Your browser is not able to display this video.
 
Ameongea ukweli mchungu kwa watawala na ccm yao. Yaani wameiba mpaka wamejisahau kama wanaiba. Na kwa kweli hii ni aibu kubwa kwa nchi na wananchi wake.

Ila mwisho wa siku, kusikitishwa tu na kulalamika haitoshi! Profesa Lipumba na wanafiki wenzake wote wanatakiwa kubadilika, na hivyo kuungana na CHADEMA ya Lissu pamoja na wapenda mabadiliko wengine kudai Katiba mpya na tume huru kweli ya uchaguzi hata ikibidi kwa kutumia nguvu ya umma kama ile iliyotokea tarehe 29.

Kinyume na hapo atakuwa anaendelea tu kutwanga maji kwenye kinu.
 
Ameongea ukweli mchungu kwa watawala na ccm yao. Yaani wameiba mpaka wamejisahau kama wanaiba.

Ila mwisho wa siku, kusikitishwa tu na kulalamika haitoshi! Profesa Lipumba na wanafiki wenzake wote wanatakiwa kubadilika, na hivyo kuungana na CHADEMA ya Lissu pamoja na wapenda mabadiliko wengine kudai Katiba mpya na tume huru kweli ya uchaguzi, hata ikibidi kwa kutumia nguvu ya umma kama ile iliyotokea tarehe 29.

Kinyume na hapo atakuwa anaendelea tu kutwanga
 
The Guilty are Afraid-James Hadley Chase
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…