Uchambuzi wangu wa mahojiano ya leo kwa Prof. Lipumba ndani ya ITV na kauli yangu.
1. Lipumba anaona kuwa kunaitajika kuwapo mabadiliko (reforms) kadha wa kadha ya uwajibikaji Serikalini, katika Katiba ya JMT na pia mabadiliko baadhi ya Sera za Uchumi, Elimu na huduma za kijamii. Michezo ipewe nafasi toka chini mashuleni na katika shule maalumu za binafsi za michezo.
2. Mabadiliko na utekelezaji wowote wa sera mpya au zilizoboreshwa ni mchakato utakaohitaji tafiti kwanza (ikibidi hata kufanya miradi ya majaribio) na kuzingatia mazingira yote husika katika marefu na mapana yake. Hapa hashabikii kabisa ahadi na ukurupukaji wa sera yeyote inayoweza kuwafurahisha wananchi leo lakini ikawa vigumu kutekelezeka.
3. Anakiri kuwa kuna ufisadi uliofanyika lakini inabidi ule uliothibitika wahusika wachukuliwe hatua mara moja. Waendesha mashitaka & mashahidi (wawakilishi wa Serikali) wawe makini katika kuandaa mashitaka na pia kuonyesha utashi wa kupambana na ufisadi
4. By implication, analawama na jinsi media ambavyo haijamtendea haki ama yeye au CUF ukilinganisha na vyama vingine vya upinzani (rejea kuibuka na kufa kwa CCJ).
5. Anasitiza kuwa katika kuwalinganisha yeye na Silaa yeye ni juu sana.
Wachambuzi hapa tunamsoma kuwa hakika anaona kuwa ni Silaa (Kichuguu) alipaswa kumuunga mkono yeye (Kilimanjaro) badala ya yeye kusukumiwa mzigo au jukumu hilo.
6. Contextually, tamko la kuwa ANAMUHESHIMU SILAA halina maana kuwa anamuunga mkono Silaa (CHADEMA) kuliko Kikwete (CCM). Maana pamoja na kutoa kasoro Serikali ya CCM pia amekosoa sana tu Sera au Mitizamo ya Silaa mf. maamuzi kuhusu ushuru wa forodha, bei za vifaa vya ujenzi, kuzingatia makubaliano yaliyopo ktk EAC na kuyaboresha na si kuyavunja tu, kutoa ahadi kubwa bila utafiti ambazo zinaweza kuwa vigumu kutekelezeka. Zaidi ya yote ingawa inaweza kuwa a bitter pill to swallow, ingawa anaikosoa Serikali, bado yeye ana matumaini kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa itaweza kuleta amani na chachu ya maendeleo. Kumuita Rais Kikwete mtani wake si tu suala la kikabila bali ametuma ujumbe muafaka kuwa upinzani si ugomvi bado wanaweza kukaa pamoja na kushauriana kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
7. Hapendi kutanguliza habari ya kuwa wataibiwa kura. Watu wajitokeze wapige kura na mchakato mzima bado unaweza kuwa wa haki na kweli. Suala la kususia Tume ya Uchaguzi halina nafasi katika agenda zake kwa sababu it just doesn't work!
8. It is not by chance, kwamba muuliza swali mmoja na mwishoni, Mtangazaji wa ITV walichukuwa nafasi nzuri kusisitiza suala la uwepo na pia credentials za nguvu za mgombea mwenza kwa CUF, kama ilivyo kwa CCM ukitofautisha na CHADEMA.
Hitimisho:
CCM ni mshindi. Vyama vingine bado hata katika kipindi hiki, hazitatosha ingawa idadi ya Wabunge toka Upinzani itaongezeka kwa kiasi kidogo