Lipumba: Miaka 65 tangu uhuru hatuna mfumo wa demokrasia katika nchi hii

Lipumba: Miaka 65 tangu uhuru hatuna mfumo wa demokrasia katika nchi hii

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
"Mwaka huu utakuwa mwaka wa 65 tangu tumepata uhuru bado hatujajenga Demokrasia, miaka saba mkoloni alikubali kuiachia Tanganyika na kupata uhuru bila kupiga watu risasi, miaka 65 hatuna mfumo wa demokrasia katika nchi hii" Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
 
Naona Lipumba ameamua kuachana kabisa na yale ya kale, na kuamua kusimama katika ukweli.

Katika ukweli huu, wotewalio wa ukweli, wapenda haki, tunasimama na kauli thabiti ya Prof. Lipumba. Tusiangalie nani anasema, bali nini amesema, kama ni cha kweli na halisia, tutasimama naye katika ukweli aunenao.

Bahati mbaya sana, hakuna ndani ya CCM amesimama na kuunena ukweli hata katikati ya uovu wa kutisha.

Lipumba na CUF yake, tumeisikia kauli yako ya kusimama katika haki.

Shekhe Ponda na Shura ya maimamu, tuliisikia kauli yao mara baada ya uovu ule.

TEC muda wote imesimama na haki za watu, hakuna aliye na mashaka.

Gwajima hajatetereka, hata walipotaka kumnajisi kupitia ile kamati ya mchongo ya kumsafisha muuji, amekana katakata, na kubakia kwenye kauli za kuetetea haki.

Mpendwa wetu, shujaa Tundu Lisu, hahitaji maelezo ya mtu, kwani uzalendo wake hauna mfanano na yeyote. Pamoha naye ni timu nzima ya uongozi wa CHADEMA.

Lakini katika laana, tuna CCM na viongozi wake wa serikali batili. Hii ndiyo laana kuu kwa Taifa letu. CCM au taasisi zake, pamoja na zile alizozipora, kama Polisi, TISS, ndiyo wamekuwa chanzo cha uovu wote usioweza kuelezeka, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji, na ufisadi.

Kila iwezekanavyo, tunaoitafuta haki, tuunganishe nguvu, na kujitenga kabisa kwa namna zote zinazowezekana na hao walio wa laana, mpaka siku watakapobadilika na kuitumikia haki.
 
"Mwaka huu utakuwa mwaka wa 65 tangu tumepata uhuru bado hatujajenga Demokrasia, miaka saba mkoloni alikubali kuiachia Tanganyika na kupata uhuru bila kupiga watu risasi, miaka 65 hatuna mfumo wa demokrasia katika nchi hii" Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
Mzee wa buguruni ulichangia kuuwa mfumo wa kidemokrasia tangu enzi za cuf hadi enzi ya cuf kukimbilia act.Umesahau enzi kukesha4 buguruni amesahau!
 
"Mwaka huu utakuwa mwaka wa 65 tangu tumepata uhuru bado hatujajenga Demokrasia, miaka saba mkoloni alikubali kuiachia Tanganyika na kupata uhuru bila kupiga watu risasi, miaka 65 hatuna mfumo wa demokrasia katika nchi hii" Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
Demokrasia inataka dhamira, ukweli na uwazi kwa sisi Afrika bado hatujafikia huko, mission ya kuivuruga CUF aliifanikisha vizuri na kwa muda mfupi wakati waasisi wake walichukua muda mrefu kukijenga chama.
 
Inaanza chamani. Ye amejenga demokrasia chamani kwake? Uhuni aliofanya chamani kwake anauzungumziaje?
 
Back
Top Bottom