Lipumba: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Ulitarajiwa Kuponya Majeraha ya Kidemokrasia, Lakini Umezidisha Maumivu

Lipumba: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Ulitarajiwa Kuponya Majeraha ya Kidemokrasia, Lakini Umezidisha Maumivu

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
"Uchaguzi Serikali Mitaa 2024 ulitarajiwa kuponya majeraha ya Kidemokrasia yaliyotokana na Uchaguzi wa 2019 na 2020 lakini umezidisha maumivu na kuwakatisha tamaa wananchi na wadau wote wa demokrasia juu ya uwezekano wa kutopata Uchaguzi huru na wa haki hapa nchini,

Matokeo ya Uchaguzi yaliyotangazwa na Waziri wa TAMISEMI tarehe 28 Novemba 2024 yaliandaliwa tarehe 26 Novemba wakati Uchaguzi ulifanyika tarehe 27 Novemba.UCHAGUZI huu umetia dosari kubwa na kuondoa kabisa MATUMAINI ya kupatikana maridhiano ya DHATI KWA UPANDE WA DEMOKRASIA. Kidonda kilichoonesha dalili za kupona na kukauka kimeanza upya kuvuja damu. Uharibifu wa Uchaguzi ulidhihirika kwenye hatua zote za mchakato."
 
Lipumba ni mmoja kati ya waliotufikisha huku
Hana haki ya kuongea chochote kuhusu utawala wa nchi.
 
Back
Top Bottom