Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)

Nashukuru sana mkuu. Nilikuwa sijui kama karanga inawahi kuharibika kiasi hicho. Sasa mbona ukiuonja huo uji wa huo mchanganyiko una ladha nzuri na ni mtamu?
 
Nashukuru sana mkuu. Nilikuwa sijui kama karanga inawahi kuharibika kiasi hicho. Sasa mbona ukiuonja huo uji wa huo mchanganyiko una ladha nzuri na ni mtamu?
Karibu mkuu, ni jukumu letu kuelimisha jamii kuhusu haya mambo.
Karanga zinaharibika mapema sana; probably huwezi kudetect kwa kuonja kwa sababu kwa kawaida kiasi cha karanga kwenye huo mseto huwa kinakuwa ni kidogo ukilinganisha na components zingine. Pia mkuu, utamu wa kitu hauna uhusiano na afya au wingi wa virutubisho kwenye chakula husika. Kuna vitu vingi tuu ambavyo vina ladha tamu sana, lakini kiafya si salama, na havina virutubisho vyovyote. Mfano soda. chifu77
 
BUTTERBUT SQUASH;LISHE YA WATOTO KUANZIA MIEZI 6 NA KUENDELEA
Posted on AUGUST 8, 2015 9:14 PM by AFYABORAKWAMTOTO
Butternut squash ni jamii ya maboga ila hili linavirutubisho zaidi na ndio mana madaktari wengi wa watoto wanashauri mtoto apewe butternut squash akifika miezi sita muda sahihi wa mtoto kuanza kujifunza kula.





Umbo lake lipo kama kibuyu ,butternut ni chakula chepesi na laini kwa mtoto anaenza kufunzwa kula solid food ,lina lainisha tumbo na kumfanya mtoto kupata choo kwa urahisi kwa wale watoto wenye matatizo ya choo (constipation )linafaa zaidi.






Jinsi ya kupikwa
Butternut squash linanjia nyingi za kupikwa hapa nitakupa baadhi ya recipes unaweza mwandalia mtoto ,ukampumzisha kula viazi kila siku


  • Chemsha kwa dakika 10-15 likiiva mwaga maji weka maziwa ya baby formula (kopo) au maziwa ya mama nusu kikombe baada ya kukamua (pump) saga pamoja tayari kuliwa.


  • Butternut squash changanya na carroti 1 chemsha pamoja ikiiva saga na tayari kuliwa


  • Viazi vitamu changanya na butternut squash chemsha pamoja na kusaga


  • Zucchini chemsha pamoja na butternut ikiiva saga tayari kuliwa

HILI NDIO ZUCCHINI LINAUMBO LA TANGO

  • Butternut,kiazi ulaya,karoti na njegere kidogo pika pamoja weka butter au olive oil kidogo ikiiva saga tayari kuliwa.


Utakapo pika chakula cha mtoto tumia butter au olive oil kwa watoto walio chini ya mwaka 1
 
Hiyo butternut kwa kiswahili yaitwaje?
Nimependa hapo pa kuchanganya na maziwa ya mama
 
Wakuu mwanangu hapendi maji, sijui nitumie mbinu gani? Ana miezi 6...
 
Wakuu mwanangu hapendi maji, sijui nitumie mbinu gani? Ana miezi 6...
Take it easy. We mnyweshe akikataa mwache ngojea muda kama lisaa ama nusu saa mpe akikataa mwache tena masaa kadhaa. Unajua wazazi wakati mwingine huwa tunawalazimisha watoto kula ama kuwapa vyakula tukijua ni watoto hapo tunakosea inabidi kumpangia mtoto ratiba ya kula ni sawa na wewe mtu akulazimishe kunywa maji au kula kipindi huna kiu au njaa utafanyaje?. Mie wangu akikataa naweka pembeni namwacha aende zake mwenyewe akiniona baadae nakunywa maji au nakula anajileta mwenyewe anapata vyake anasepa tena. Tumia ratiba yako ya kunywa maji kwa mwanao ikiwa hana tatizo lolote.
 
 
ngoja nijaribu huu utaratibu
 
zingatia ucje ukaweka chumv nyingi kwenye cchakula cha mtot figo zake hazina uwezo mkubwa wakuiondoa Huyo chumvi mwilin inatakiwa use unaihic kwa mbal xana
 
Jamani wadau mbona mmeikimbia hii mada au watoto zenu wamekua siku hizi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…