Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)

Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)

Me wa kwangu ananishangaza sana huyu pc kali.
Ana miezi nane kasoro uji hataki na maziwa yangombe ataki
Anapenda ugali na mchuzi wa maharagwe au mboga yoyote yenye mchuzi mchuzi.
Kuna siku alinichekesha sana mke alinunua vichwa na miguu ya kuku ya kukaangwa.basi nikachukua mguu wa kuku nikampa alihangaika nao wewee ukidondoka au ukimnyanganya anamwaga kilio kama kafinywa shavu
 
Habari zenu

Leo nimeona ni vyema wana jikoni na wazazi tujadili na tubadilishane mawazo kuhusu lishe za watoto wetu kuanzia umri wa miezi 6 hadi mwaka.....

Nini madhumuni hasa

1)kwa wale watoto ambao hawapendi kula au hatujatambua bado nini wanapenda lakini kuna mzazi yeyote ameona chakula flani kime work kwake basi tu share nasi kujaribu kama kitapendwa pia....


2)tujuzane trick gani unatumia wakati wa kumlisha mtoto binafsi mimi huwa namfunga kwenye kiti chake alafu nampa kijiko au kipaja cha kuku sasa wakati anafungua mdomo kutafuna alichokikamata mie namuwahi kupitisha kijiko cha chakula hii inasaidia sana na tricks nyengine tutazidi kujuzana...


Karibuni wote tujadili au tupia recipe zako.


===============================


Lishe (1) - UJI WA OATS NA NDIZI/APPLE


Mahitaji

Oats kiasi

Apple 1 au ndizi ya kuwiva...

Maziwa...

Sukari (sio lazima)...

Namna ya kutaarisha

Chemsha maji

Weka oats acha zichemke hadi kuwiva

Ponda ponda ndizi vizuri weka maziwa kidogo ipondeke vizuri....

Mimina kwenye oats alafu weka na maziwa acha ichemke kidogo kwa dakika 3

Epua mlishe mtoto.....



Lishe (3) - WALI WA YAI

Mahitaji

Yai 1....tumia kiini tu

Siagi kidogo

Mchele....

Namna ya kutaarisha...

Pika wali kama wa kawaida ila weka maji mengi uwe laini bwabwa wengine wanaita bondo

Ukikaribia kuwiva weka yai ulolivunja koroga haraka haraka uchanganyike vizuri

Weka siagi na chumvi kidogo ukipenda....

Epua mlishe mtoto....


Lishe (3) - KAROTI NA KUKU


Mahitaji

Karoti

Kuku kiasi


Namna ya kutaarisha

Chemsha kuku hadi kuwiva iwe na supu kidogo

Weka karoti na subiria kuwiva...

Toa kuku pembeni alafu mchambue mifupa tupa

Weka katika blenda kuku na katoti na supu yako saga

Tayari kwa kumlisha mtoto

Ukipendeza waweza weka na viazi



Endelea kufuatilia mjadala kwa ushauri na lishe zaidi....
Nyo nyo
 
Back
Top Bottom